Nijuze Habari

Matokeo Red Arrows vs Simba SC

Filed in Michezo by on 05/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KLABU ya Simba kwa mara ya kwanza imefanikiwa kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup).

Licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows kwenye mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Jijini Lusaka Zambia Simba imefanikiwa kufuzu hatua hiyo ya makundi.

Mabao ya Red Arrows yamefungwa na Ricky Banda dakika ya 44 na Saddam Phiri dakika ya 47, huku bao pekee la Simba SC limefungwa na Hassan DIlunga dakika ya 67.

Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam imefuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 kufuatia ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliofanyika Jumapili iliyopita Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Kufuzu kwa Simba SC katika hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho kunaifanya Tanzania ifikishe pointi 23 kwenye rank ya Afrika.

Baada ya kufanikiwa kufuzu hatua hiyo ya makundi Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Pablo Franco Martín amesema kuwa amefurahi kwa sababu malengo ya kuendelea kuwa kwenye michuano ya Kimataifa yametimia na sasa Klabu hiyo imefuzu hatua ya makundi.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.