LIVE AL AHLY VS WYDAD AC Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 3:00 Usiku. 

Matokeo Ruvu Shooting FC vs Simba SC November 19,2021

Filed in Michezo by on 19/11/2021 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao, Ruvu Shooting FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere akifunga mawili dakika ya 17 na 36 huku bao la tatu likifungwa na Mtanzania Kibu Denis kwenye dakika ya 44.

Bao pekee la Ruvu Shooting ambao waliutumia Uwanja wa CCM Kirumba kama Uwanja wa nyumbani limefungwa na Elias Maguri mshambuliaji wa zamani wa Simba na Klabu kadha wa kadha ndani na nje ya nchi Elias Maguli dakika ya 71.

Kwa ushindi huo Simba inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi sita (6) na kuendelea kushikilia nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi, ikizidiwa pointi moja na watani zao Young Africans SC ambao wamecheza mechi tano (5), huku Ruvu Shooting ikibaki na pointi zao sita baada ya mechi sita (6) ikishuka hadi nafasi ya 11.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara zilizchozezwa leo, bao pekee la Benedictor Jacob dakika ya 46 limewapa Coastal Union FC ya Tanga ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania FC kwenye Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Ushindi huo unaifanya Coastal ifikishe pointi saba (7) baada ya kucheza mechi sita (6) na kusogea hadi nafasi ya 10, wakati Polisi Tanzania ikibaki na pointi zake 10 baada ya mechi sita (6) kwenye nafasi ya tatu ya Msimamo.

Tanzania Prisons FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya Kwanza FC kwenye Uwanja wa Mandela, Sumbawanga Mjini Rukwa kwenye mchezo uliopigwa mapema leo.

Mabao ya Prisons yamefungwa na Dotto Shabani dakika ya 28 na Jeremiah Juma dakika ya 90 huku bao pekee la Mbeya Kwanza FC likifungwa na Dedastus Mwihambi aliyejifunga kwenye dakika ya 25.

Baada ya ushindi huo Prisons inapanda hadi nafasi ya 12 kwenye Msimamo wa Ligi kwa michezo sita (6) na Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake saba (7) za mechi sita huku ikishuka hadi nafasi ya saba kutoka ya sita.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *