telegram Nijuze Habari

Matokeo Simba SC vs ASES Mimosas

Filed in Michezo by on 13/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Simba SC leo Jumapili February 13,2022 wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Bao la mapema lilijazwa kimiani na Pape Ousmane Sakho dakika ya 12 kwa pasi ya Shomari Kapombe lilidumu mpaka muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili ASEC Mimosas walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Aziz Stephan ambaye alitumia vema makosa ya safu ya ulinzi wa Simba chini ya Joash Onyango.

Bao la pili kwa Simba lilipachikwa na Shomari Kapombe ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 78 baada ya Golikipa wa ASES kumvuta miguu mshabuliaji wa Simba Yusufu Mhilu.

Iliwachukua dakika tatu mbele Simba kupachika bao la tatu kupitia kwa Peter Banda ambaye alionyeshwa kadi ya njano kutokana na kuvua jezi wakati anashangilia.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *