Nijuze Habari

MATOKEO | Simba SC vs Azam FC Mapinduzi Cup 2022

Filed in New by on 13/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

KLABU ya Simba SC imefanikiwa kuibuka Bingwa wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2022 baada ya kuichapa Azam FC bao 1-0.

Bao la ushindi lililoipa Klabu hiyo Ubingwa limefungwa na Mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati baada ya Golikipa wa Azam FC Mathias Kigonya kumchezea rafu Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Pape Ousmane Sakho.

Klabu hiyo imechukua Kombe hilo bila kuruhusu bao hata moja, hii ni rekodi mpya kwenye mashindano haya.

Aidha Klabu hiyo pia imefanikiwa kubeba tuzo zote za Mapinduzi Cup 2022 ambapo tuzo ya Golikipa Bora imeenda kwa Aishi Manula, Mchezaji Bora wa Fainali amechukua Honock Inonga.

Tuzo nyingine ni ya Mchezaji Bora ambapo imechukuliwa na Pape Ousmane Sakho, Mfungaji Bora hiyo imeenda kwa Meddie Kagere.

Hapa ni kombe likakabidhiwa kwa nahodha wa mabingwa hao wa Mapinduzi 2022 John Bocco, likiambatana na kitita cha shilingi Milioni 25, huku Mshindi wa Pili Azam FC akibeba Milioni 15.

 

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.