Nijuze Habari

MATOKEO Simba SC vs Azam FC

Filed in Michezo by on 01/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA watetezi, Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ni kiungo wa kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute aliyefunga bao la kwanza la Simba SC dakika ya 67, kabla ya Pape Ousmane Sakho kufunga la pili dakika ya 72, huku bao pekee la Azam FC likifungwa na mshambuliaji Rodgers Kola dakika ya 79.

Baada ya ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 24 baada ya michezo 10, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na watani za Young Africans SC, ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 15 za michezo 11 katika nafasi ya saba.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.