Nijuze Habari

Matokeo Simba SC vs Geita Gold December 01,2021

Filed in Michezo by on 01/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza furaha kwa mashabiki wao baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold kwenye katika wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Peter Banda dakika ya tisa na mzawa, Mzamiru Yassin dakika ya 57, wakati la Geita Gold limefungwa na kiungo pia, Juma Mahadhi dakila ya 66.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 17, ingawa inabaki na nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na watani wa jadi, Young Africans SC baada ya timu zote kucheza mechi saba kuelekea mechi baina yao (DarDeby) December 11 hapo hapo Mkapa.

Geita Gold yenyewe baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake tano za mechi saba pia katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ikiizidi pointi tatu tu Mtibwa Sugar inayoshika mkia.

Haya hapa ni matokeo ya mechi zote za raundi ya saba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu wa 2021/2022.

FT Ruvu Shooting FC 2-1 Kagera Sugar FC
FT Mbeya City FC 2-2 KMC FC
FT Tanzania Prisons FC 3-1 Namungo FC
FT Dodoma Jiji FC 0-0 Coastal Union FC
FT Biashara United FC 1-1 Polisi Tanzania
FT Mbeya Kwanza FC 0-2 Young Africans
FT Azam FC 1-0 Mtibwa Sugar FC
FT Simba SC 2-1 Geita Gold FC

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.