Nijuze Habari

Matokeo Simba SC vs Mbeya City

Filed in New by on 17/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application
MABINGWA watetezi, Simba SC wamepoteza Mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu wa 2021/2022 baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji, Mbeya City Leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Bao pekee la Mbeya City limefungwa na mshambuliaji Paul John Nonga dakika ya 41 akimchambua kwa ustadi kipa namba moja Tanzania, Aishi Salum Manula baada ya kumtoka beki Mkongo, Hennock Inonga Baka ‘Varane’.

Mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mutshimba Mugalu aligongesha mwamba wa mkwaju wa penalti dakika ya na Nahodha, John Raphael Bocco alipojaribu kwenda kumalizia ndani ya sita, kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ alidaka.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki Juma Shemhuni kuangukia mpira wakati akijaribu kuokoa shambulizi la winga wa Simba, Kibu Denis.
Kwa zaidi ya nusu ya mchezo huo, Mbeya City ilicheza pungufu baada ya beki wake, Mpoki Mwakinyuke kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 43 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 19 baada ya michezo 12 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi 5 na Simba SC ambayo imecheza mechi 11 – wote wakiwa nyuma ya Yanga wenye pointi 32 baada ya Michezo 12.
Mchezo mwingine, Polisi Tanzania FC wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare tasa (0-0) na Namungo FC kwenye Mchezo wa mapema uliofanyika kwenye Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi.
telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.