Nijuze Habari

Matokeo Simba SC vs Mtibwa Sugar FC

Filed in New by on 22/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

WENYEJI, Mtibwa Sugar wameambulia sare dhidi ya Mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mangunu Complex, Turiani mkoani Morogoro.

Kwa Matokeo hayo Mtibwa Sugar inafikisha pointi 12 baada ya michezo 13 na kusogea nafasi ya 13, wakati Simba SC inafikisha pointi 25 baada ya michezo 12, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi saba na watani wao wa jadi Young Africans SC baada ya timu zote kucheza mechi 12.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Azam FC imewatandika wenyeji, Tanzania Prisons mabao 4-0, mabao hayo yamefungwa na Tepsi Evance dakika ya 27, Ismail Aziz Kader dakika ya 68, Ibrahim Ajibu dakika ya 70 na Justin Zullu dakika ya 82, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mchezo wa tatu wa leo Biashara United imelazimishwa sare ya bila kufungana na Geita Gold  ya Geita kwenye Uwanja wa Karume Mjini Musoma mkoani Mara.

Kwa Matokeo hayo Azam FC inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nne, ikizidiwa pointi moja na Mbeya City iliyopo nafasi ya tatu, hii ni  baada ya timu zote kucheza michezo 13.

Tanzania Prisons yenyewe inabaki na pointi zake 11 saa ya michezo 13 na sasa inahamia mkiani, huku Biashara United ikifikisha pointi 11 baada ya michezo 13 ikiwa nafasi ya 14 na Geita Gold sasa imefikisha pointi 14 baada ya michezo 13 pia ikiwa nafasi ya 10.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.