Nijuze Habari

Matokeo Simba SC vs Namungo FC

Filed in Michezo by on 10/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.

Mabao ya Simba SC kwenye Nusu Fainali hiyo ya Pili yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere dakika ya 15 na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 49.

Baada ya ushindi huo Simba SC Sasa watakutana na Azam FC waliowavua Ubingwa Young Africans SC kwa mikwaju ya penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 za mchezo huo wa Nusu Fainali ya Kwanza.

Mchezo huo wa Fainali unarajiwa kuchezwa Alhamisi ya January 13,2022 Saa 20:15 Kwenye Uwanja huo huo wa Amaan Mjini Zanzibar.

Aidha Bingwa wa Michuano hiyo safari hii atapata 25M, tofauti na msimu uliopita ambapo Bingwa alipata 15M na Mshindi wa pili atapata 20M, tofauti na msimu uliopita ambapo alipata 10M.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.