Nijuze Habari

Matokeo Simba vs Yanga (Ngao ya Jamii 2021)

Filed in Michezo by on 25/09/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022 wa (Ngao ya Jamii).

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam umeisha kwa bao la mkongomani Fiston Kalala Mayele lililofungwa kwenye dakika ya 11 ya mchezo huo.

Kiungo mkata umeme wa Simba SC, Taddeo Lwanga raia wa Uganda alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Kwa matokeo hayo Yanga ndio Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2021 na sasa imefikia rekodi ya Simba SC ya kutwaa Ngao ya Jamii mara ya sita.

Ushindi huo unaamsha ari na hamasa kwa mashabiki wa Yanga pamoja na benchi nzima la ufundi likiongozwa na Nasredine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze baada ya presha kubwa iliyokuwa inamkabili.

Klabu hiyo imelipa kisasi kwa Simba baada ya kufungwa kwenye mchezo wao wa mwisho waliokutana kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), July 25, 2021, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

Baada ya mchezo huo Simba na Yanga zitakutana tena mwaka huu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara December 11.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.