telegram Nijuze Habari

MATOKEO Tanzania U17 vs Botswana U17

Filed in Michezo by on 20/03/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MATOKEO Tanzania U17 vs Botswana U17

TIMU ya Taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 imefanikiwa kwenda raundi ya tatu Kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Botswana leo Jumapili March 20,2022 kwenye Uwanja wa Francistown mjini Francistown.

Mabao ya Tanzania yamefungwa na Neema Kinega dakika ya 28 na Clara Luvanga matatu dakika za 62, 63 na 81.

Kwa matokeo hayo Tanzania inafuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 11-0 kufuatia kuwachapa Botswana 8-0 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Zanzibar.

Sasa Tanzania itacheza dhidi ya Burundi kuwania kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya India baadae mwaka huu.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *