Nijuze Habari

Matokeo Tanzania vs Benin (Kufuzu Kombe la Dunia)

Filed in Michezo by on 07/10/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

TIMU ya taifa ya Tanzania imepoteza mchezo wa kwanza wa kundi lake J kufuzu Kombe la Dunia mwakaki nchini Qatar baada ya kuchapwa 1-0 na Benin nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Bao pekee la Benin limefungwa na mshambuliaji wa anayecheza klabu ya Brest inayoshiriki Ligue 1 ya Ufaransa, Steve Michel Mounié dakika ya 70.

Kwa matokeo hayo, Benin inajitanua kileleni mwa msimamo ikifikisha pointi saba katika michezo mitatu ya mwanzo, ikifuatiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yenye pointi tano baada ya kuichapa Madagascar mabao 2-0 leo Jijini Kinshasa.

Tanzania inayobaki na pointi zake nne, sasa inaangukia nafasi ya tatu mbele ya vibonde, Madagascar waliopoteza michezo yote mitatu ya mwanzo, moja nyumbani dhidi ya Benin na mbili ugenini kwa DRC na Tanzania.

Baada ya mchezo wa leo Tanzania itasafiri kwenda Cotonou kwaajili ya mchezo wa marudiano na Benin Jumapili hii ya October 10,2021, huku DRC ikiifuata Madagascar.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.