Nijuze Habari

Matokeo droo ya UEFA Champions League baada ya mabadiliko

Filed in Michezo by on 13/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya Chelsea watacheza dhidi ya Mabingwa wa Ufaransa Lille katika Michuano ya kufuzu hatua ya robo Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya baada ya droo ya mechi hizo za mtoano kufanyika kwa mara ya pili.

Tatizo la kiufundi lilisababisha makosa katika droo ya awali ambayo UEFA walisema kuwa imekataliwa.

Mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City watacheza dhidi ya Sporting Lisbon ya Portugal huku washindi mara sita Liverpool wakicheza dhidi ya mabingwa mara tatu wa Italia Inter Milan.

Manchester United wao watacheza dhidi ya Mabingwa wa Uhispania Atletico de Madrid, huku Real Madrid ikicheza dhidi ya PSG ya Ufaransa.

Orodha mpya mechi za Klabu Bingwa Ulaya

➡️FC Salzburg/Australia vs FC Buyern Munich/Germany
➡️Sporting Club/Portugal vs Manchester City/England
➡️SL Benfica/ Portugal vs Ajax Amstadam/Netherland
➡️ Chelsea FC/England vs vs Lille/France
➡️Atletico de Madrid/Spain vs Manchester United/England
➡️Villarreal CF/Spain vs Juventus/Italy
➡️ Internazionale Milan/Italy vs Liverpool/England
➡️Paris Saint- Germany/France vs Real Madrid/Spain

Kabla ya droo hiyo kurudiwa upya Klabu ya Manchester United ilipangwa dhidi ya Villarreal CF lakini hiyo haikuweza kukubalika chini ya sheria za Michuano hiyo kwa sababu walikuwa katika kundi moja hali iliyofanya droo hiyo kurudiwa upya.

Katika taarifa hiyo, UEFA ilisema kuwa droo hiyo haitakubalika na kuongezea kuwa kutokana na tatizo la kiufundi na programu ya mtoaji huduma wa nje ambaye huwapatia maelezo maafisa kuhusu ni timu gani zinazopaswa kucheza dhidi ya zingine.

Makosa yalifanyika katika droo ya Michuano ya Klabu Bingwa katika raundi ya kufuzu kwa robo Fainali.

Mechi za kwanza zinatajiwa kuchezwa kati ya tarehe 15, 16, 22 na 23 mwezi February huku mechi za marudiano zikitarajiwa kuchezwa tarehe 8, 9, 15 na 16 mwezi March 2021.

Mabadiliko Makuu yaliyofanywa msimu huu ni kuwa bao la ugenini limeondolewa huku timu zikilazimika kucheza muda wa ziada baada ya dakika 180.

Iwapo timu hizo zitashindwa kupata mshindi wa jumla baada ya nyongeza ya dakika 30, basi timu zitashiriki katika mikwaju ya penalti.

Fainali ya msimu huu itachezwa katika uwanja wa ST Petersburg nchini Urusi May 28,2021.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.