Nijuze Habari

Matokeo ya Ligi Kuu leo Jumatatu September 27,2021

Filed in Michezo by on 27/09/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KLABU ya Namungo FC imeanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2021/2022 baada ya kuibuka ma ushindi wa 2-0 dhidi ya wageni wa Ligi Geita Gold FC ya Geita jioni ya leo kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Mabao ya Namungo FC, yamefungwa na Shiza Ramadhan Kichuya dakika ya 13 na Relliant Lusajo dakika ya 81.

Michezo mingine ya Ligi Kuu leo Jumatatu, Coastal Union FC imetoka sare ya bao 1-1 na Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wageni wakitangulia kwa bao la beki Mghana, Daniel Amoah dakika ya 49, kabla ya Hance Masoud kuwasawazishia wenyeji kwenye dakika ya 90.

Na wageni wengine kwenye Ligi Mbeya Kwanza FC kutoka Mbeya wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao pekee la William Edgar dakika ya 50 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.