Nijuze Habari

Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara leo Jumanne September 28,2021

Filed in Michezo by on 28/09/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara leo Jumanne September 28,2021

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara jioni ya leo.

Nahodha na mshambuliaji tegemezi wa Klabu hiyo, John Raphael Bocco amekuwa na bahati mbaya na kusababisha kulaumiwa na mashabiki baada ya kuikosesha ushindi timu hiyo kufuatia mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Mganda, James Ssetuba dakika ya 90.

Mechi nyingine za Ligi Kuu zilizchozezwa leo Jumanne, bao pekee la Cleophace Mkandala dakika ya 33 limewapa wenyeji, Dodoma Jiji FC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting FC mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, bao la Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei limeipa Mbeya City ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.