telegram Nijuze Habari

MATOKEO ya SENSA Tanzania 2022

Filed in Habari by on 31/10/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MATOKEO ya SENSA Tanzania 2022

MATOKEO ya SENSA Tanzania, Matokeo ya SENSA 2022, SENSA ya Watu na Makazi, SENSA ya Tanzania, Matokeo ya SENSA, Matokeo SENSA Tanzania, SENSA Tanzanian, Matokeo ya SENSA Zanzibar, Matokeo ya SENSA Dar es Salaam, Matokeo ya SENSA Mwanza.

MATOKEO ya SENSA Tanzania 2022

MATOKEO ya SENSA Tanzania 2022

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa idadi ya Watanzania ni milioni 61.7 mpaka kufikia October 31, 2022.

Ameyasema hayo katika Uzinduzi rasmi wa matokeo ya SENSA ya watu na Makazi ya mwaka 2022 uliofanyika Makao Makuu ya nchi hiyo, Dodoma.

”Ninawatangazia rasmi kuwa Tanzania ina idadi ya watu wapatao 61,741,120 ” Alisema Rais Samia.

Kati ya idadi hiyo 59,851,357 wapo Tanzania bara na watu 1,889,773 wako Tanzania Zanzibar.

Kati ya idadi hiyo ya Watanzania wanawake ni 31,687,990 sawa na asilimia 51, huku wanaume wakiwa asilimia 49 ya watu wote.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 44,928,923 hii inaonesha kumekuwepo na ongezeko la watu 16,812,197 sawa na ongezeko la 3.2% kati ya ongezeko la mwaka 2012 na mwaka 2022.

”Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, ya mwaka 2022, kuhusu Matokeo ya Idadi ya watu Duniani ya mwaka 2012, Dunia ilikuwa na watu bilioni 7 na ilitarajiwa kuongezeka hadi kufikia bilioni nane mwaka huu 2022, hili ni ongezeko la watu bilioni moja katika kipindi cha miaka 10”. Amesema Rais Samia.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa mwaka 2022 Bara la Afrika hususani katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara lina Jumla ya watu bilioni 1.2 idadi inayokadiriwa kuongezeka hadi kufikia watu Bilioni 2.1 ifikapo mwaka 2050.

Taarifa zaidi soma HAPA

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *