Nijuze Habari

Matokeo ya Simba SC vs Mlandege FC

Filed in New by on 07/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi licha ya sare ya 0-0 na wenyeji, Mlandege FC leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kwa matokeo hayo, Simba inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake nne, mbili zaidi ya Mlandege FC hivyo inatinga Nusu Fainali na itakutana na mshindi wa pili wa Kundi A Jumatatu.

Tayari Kundi A zote Azam na Namungo zimefuzu Nusu Fainali baada ya kila timu kukusanya pointi nne.

Namungo imekamilisha mechi zake, wakati Azam FC wanacheza mechi ya mwisho dhidi ya Yosso Boys kesho.

Azam FC na Namungo FC za kundi A zote zimefuzu hatua hiyo tayari, huku Simba SC na Young Africans SC wamesubili mechi ya kesho Kati ya Azam FC vs Yosso Boys ndipo wajue watakutana na nani Kati ya Namungo FC au Azam FC.

Ratiba inaonesha kuwa mshindi wa kwanza wa Kundi A Kati ya Azam FC na Namungo atacheza dhidi ya mshindi wa kwanza wa Kundi B, ambaye ni Young Africans SC wakati mshindi wa pili wa Kundi A, atacheza dhidi ya mshindi wa kwanza wa Kundi C ambaye ni Simba SC.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.