Nijuze TV App Nijuze Habari Teregram Channel Nijuze Habari WhatsApp group Nijuze Habari Instagram
telegram Nijuze Habari

Matokeo ya Yanga vs Mbeya City

Filed in Michezo by on 05/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

WENYEJI, Young Africans SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Sare inayoiongezea alama moja kila timu, na inaifanya Young Africans ifikishe pointi 36 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya wote kucheza michezo 14.

Mbeya City wao wanafikisha pointi 23 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Azam FC.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Kagera Sugar imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Erick Mwijage dakika ya 20 na 73, wakati bao pekee la Coastal Union likifungwa na Vincent Abubakar kwenye dakika ya 54.

Kagera Sugar inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union ikibaki na pointi zake 17 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza michezo 14.

KMC FC wao wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Biashara United kwenye Uwanja wa Azam Complex, (Chamazi) nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

KMC inafikisha pointi 16 katika nafasi ya 10 na Biashara United inafikisha pointi 12 katika nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya timu zote kucheza mechi 14.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *