Nijuze Habari

Matokeo ya Yanga vs Mbuni FC, Mchezo wa Kirafiki

Filed in New by on 19/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Klabu ya Young Africans SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC ya Monduli katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Mabao yote ya Young Africans yamefungwa na kiungo wa kimataifa wa DR Congo, Mukoko Tonombe kwa mikwaju ya penati kipindi cha pili.

Bao la kwanza limepatikana baada ya beki wa Mbuni kuunawa mpira kwenye boksi dakika ya 56 na la pili ni baada ya Mkongo mwenzake, Chico Ushindi kuangushwa kwenye boksi dakika ya 82.

Huu unakuwa mchezo wa kwanza wa Mchezeshaji Chico Ushindi baada ya kusajiliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka TP Mazembe ya kwao, Kinshasa DR Congo.

Klabu ya Young Africans SC imeutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wake ujayo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania FC.

Mchezo huo inatarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.