Nijuze Habari

Matokeo Yanga SC vs Azam FC, October 30,2021

Filed in Michezo by on 30/10/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABAO ya washambuliaji Wakongo, Fiston Kalala Mayele na Jesus Ducapel Moloko yameipa ushindi wa mabao 2-0 Klabu ya Young Africans SC dhidi ya Azam FC, mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Bao la kwanza la Young Africans lilifungwa na Fiston Kalala Mayele dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya beki mzawa, Kibwana Shomari.

Bao la pili na la ushindi la Young Africans SC lilifungwa na Jesus Moloko dakika ya 72 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne.

Ushindi huo unaifanya Young Africans SC kufikisha jumla ya pointi 12 baada ya kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Dodoma Jiji FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.

Azam FC yenyewe baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake nne baada ya kucheza mechi nne na huu ndio Msimamo wa NBC Premier League baada ya michezo miwili ya October 30,2021.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.