Matokeo Yanga SC vs Biashara United FC

Filed in Michezo by on 15/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

Matokeo Yanga SC vs Biashara United FC

Yanga SC, Biashara United FC, Young Africans SC, Biashara Mara FC, Matokeo hatua ya 16 Bora, ASFC, Kombe la Shirikisho, Kombe la FA, Kombe la Azam Sports Federation,  Matokeo Azam Sports Federation Cup, Matokeo Yanga SC vs Biashara United FC, Matokeo ya Yanga dhidi ya Biashara United FC.

Klabu ya Young Africans SC, imefanikiwa kutinga robo Fainali ya Michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora uliopigwa Katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mabao mawili ya Ushindi wa Young Africans yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa beki anayeweza kucheza kama Kiungo Yannick Bangala dakika ya 22 na Mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 28.

Bao pekee la Biashara United lilifungwa na Mshambuliaji Mkenya, Collins Opare dakika ya 38 baada ya kiungo Khalid Aucho kuchelewa kuondoa hatari langoni mwa Klabu hiyo.

Katika mchezo uliotangulia, Polisi Tanzania ilifanikiwa pia kwenda Robo Fainali ya Michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons.

Mabao hayo ya ushindi wa Polisi Tanzania yamefungwa na Said Khamis dakika ya 40 na Daruwesh Saliboko dakika ya 83, mchezo uliofanyika Katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya.

Timu zingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0 na Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0.

Hatua ya 16 Bora ya Azam Sports Federation Cup itakamilishwa kesho Jumatano kwa michezo mingine miwili kati ya Pamba ​​vs Dodoma Jiji​​ni Mwanza na Ruvu Shooting vs Simba SC Jijini Dar es Salaam.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *