Nijuze Habari

Matokeo Yanga SC vs Biashara United FC

Filed in Michezo by on 26/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

WENYEJI wa mchezo, Young Africans SC wametoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Biashara walitangulia kwa bao la Atupele Green Jackson dakika ya kwanza tu, kabla ya mshambuliaji Fiston Kalala Mayele kuisawazishia Yanga SC dakika ya 39 kwa bao zuri la til-tak akimalizia krosi ya Mkongomani mwenzake, beki Djuma Shabani kutoka upande wa kulia.

Kiungo mkongwe Mrundi, Said Ntibanzokiza akaifungia bao la ushindi Young Africans dakika ya 78 kwa mkwaju wa penati baada ya beki Abdulmajid Mangaro kumsukuma winga Mkongo, Jeses Moloko Ducapel.

Baada ya matokeo hayo, Young Africans inafikisha pointi 26 katika michezo 10 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.

Biashara United yenyewe baada ya kipigo cha leo ambacho ni cha tatu mfululizo ikitoka kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar na 1-0 dhidi ya Coastal Union, inabaki na pointi zake nane baada ya mechi 11 katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.