Nijuze Habari

MATOKEO Yanga SC vs Dodoma Jiji FC

Filed in Michezo by on 31/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

VINARA wa NBC Premier League, Young Africans SC wamefunga mwaka 2021 ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye mchezo wa Ligi hiyo leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkala Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Wakongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 41, Jesus Ducapel Moloko dakika ya 56, Justine Billary aliyejifunga dakika ya 69 na kiungo Mganda Khalid Aucho dakika ya 81.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 29 baada ya michezo 11, pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC wanaofuatia katika nafasi ya pili ambao hata hivyo wana michezo miwili mkononi.

Dodoma Jiji FC wao wanabaki na pointi zao 16 baada ya michezo 11 pia katika nafasi ya sita.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.