telegram Nijuze Habari

MATOKEO Yanga SC vs KMC FC, March 19,2022

Filed in Michezo by on 19/03/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MATOKEO Yanga SC vs KMC FC, March 19,2022

Ratiba ya NBC Premier League, Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Ratiba ya Tanzania Bara, NBC Premier League, Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, NBC Premier League, Yanga SC, Young Africans SC vs KMC FC, Young Africans Sports Club, Jangwani Dar es salaam, Somalia vs Yanga, Somalia vs Young Africans SC, KMC FC, Kinondoni Municipal Council, Yanga SC vs KMC FC.

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) Klabu ya Young Africans SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu baada ya kuichapa KMC FC mabao 2-0, Mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, ulishuudiwa Young Africans ikijipatia bao la kwanza kupitia beki wa zamani wa timu hiyo, Andrew Vincent ‘Dante’ aliyejifunga kwenye dakika ya 38 akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira uliounganishwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.

Bao la Pili na la ushindi kwa Young Africans limefungwa na beki Mkongo, Djuma Shaaban kwenye dakika ya 52.

Kwa ushindi huo, Young Africans inafikisha pointi 48 baada ya kucheza Michezo 18 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi 11 zaidi ya Mabingwa watetezi Simba SC ambao wana mechi moja mkononi.

KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 22 baada ya kucheza Michezo 18 ikiwa kwenye nafasi ya saba ya Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Aidha Mchezo huo ilikwenda sambamba na sherehe za kuzimisha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.

 

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *