Matokeo Yanga SC vs KMKM SC

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


MABINGWA watetezi, Young Africans SC wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi licha ya sare ya 2-2 na wenyeji, KMKM leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Heritier Makambo dakika ya 45 na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah dakika ya 81, wakati ya KMKM yamefungwa na Adam Ibrahim Abdallah dakika ya 54 na Kheri Makame Jecha dakika ya 3 Kati ya zilizoongezwa baada ya dakika 90 za kawaida kuisha..
Kwa matokeo hayo, timu zote zinamaliza mechi za Kundi B na pointi nne kila moja baada ya mechi mbili, lakini Yanga wanakwenda Nusu Fainali kwa kuwazidi wastani wa mabao KMKM wameruhusu bao moja zaidi ya Young Africans SC.
Azam FC na Namungo FC za kundi A zote zimefuzu hatua hiyo tayari, huku Simba SC na Young Africans SC wamesubili mechi ya kesho Kati ya Azam FC vs Yosso Boys ndipo wajue watakutana na nani Kati ya Namungo FC au Azam FC.
Ratiba inaonesha kuwa mshindi wa kwanza wa Kundi A Kati ya Azam FC na Namungo atacheza dhidi ya mshindi wa kwanza wa Kundi B, ambaye ni Young Africans SC wakati mshindi wa pili wa Kundi A, atacheza dhidi ya mshindi wa kwanza wa Kundi C ambaye ni Simba SC.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: KMKM SC, Makundi Mapinduzi Cup 2022, Mapinduzi Cup, Mapinduzi Cup 2022, Matokeo ya Mapinduzi Cup 2022, Matokeo Yanga SC vs KMKM SC, Ratiba ya Mapinduzi Cup, Yanga SC