telegram Nijuze Habari

Matokeo Yanga SC vs Mtibwa Sugar FC

Filed in Michezo by on 23/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

Matokeo Yanga SC vs Mtibwa Sugar FC

Ratiba ya NBC Premier League, Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Ratiba ya Tanzania Bara, NBC Premier League, Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, NBC Premier League, Yanga SC, Mtibwa Sugar FC, Young Africans SC vs Mtibwa Sugar FC, Young Africans Sports Club, Jangwani Dar es salaam, Yanga, Mtibwa Sugar.

VINARA, Young Africans SC wamekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar, Mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.

Mabao ya Young Africans yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzonkiza dakika ya 45+5 na mshambuliaji Mkongomani, Fiston Kalala Mayele dakika ya 66.

Kwa ushindi huo, Young Africans inakamilisha Michezo 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 39, Pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wamecheza Michezo 15.

Mtibwa Sugar baada ya kipigo cha kwanza nyumbani, Manungu msimu huu wanabaki na pointi zao 12 baada ya Michezo 15 wakiwa nafasi ya 15 ya Ligi ya timu 16, ambayo mwishowe mbili zitateremka moja kwa moja na mbili kwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *