Nijuze Habari

Matokeo Yanga SC vs Polisi Tanzania FC

Filed in Michezo by on 23/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

VINARA, Young Africans SC wameendelea kuwapa raha mashabiki wao baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, wahamiaji Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Bao pekee la Young Africans SC limefungwa kiungo mshambuliaji, Dickson Ambundo aliye katika msimu wa kwanza baada ya kusajiliwa kutoka Dodoma Jiji FC baada ya kumalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala dakika ya 64.

Kwa ushindi huo, Young Africans inafikisha pointi 35 baada ya michezo 13 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 10 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.

Polisi Tanzania wao wanabaki na pointi zao 18 za mechi 13 sasa katika nafasi ya tano.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Namungo FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Mabao ya Namungo FC yamefungwa na  Obrey Chirwa dakika ya 38 na Relliant Lusajo mawili dakika ya 81 na 85, wakati bao pekee la Coastal Union alijifunga Abdulmik Zacharia dakika ya 46.

Namungo inafikisha pointi 17 baada ya michezo 13 na kusogea nafasi ya sita, ikiishushia Coastal nafasi ya saba ambayo inabaki a pointi zake 17 za mechi 13 pia.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.