Nijuze Habari

Matokeo Yanga vs Mbao FC, Azam Sports Federation Cup (ASFC)

Filed in Michezo by on 29/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MCHEZO wa kombe la shirikisho la Azam Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya 32 kati ya Young Africans SC dhidi ya Mbao FC umekamilika kwa wanyeji Young Africans kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee la Young Africans, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza limefungwa na Mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 54 kwa kichwa akimalizia krosi maridadi ya kiungo Farid Mussa Malik.

JINSI ya kushinda Mamilioni na ZEPPELIN SOKABET

Baada ya ushindi huo Young Africans imesonga mbele kwenye michuano hiyo na kutinga hatua ya 16 bora ikiunganana na timu za Baga Friends FC na Polisi Tanzania FC.

Zingine zilizofuzu hatua ya 16 bora ni Dodoma Jiji FC, Pamba FC, Namungo FC, Azam FC, Coastal Union FC na Ruvu Shooting FC.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.