Nijuze Habari

Matokeo Yanga vs Tanzania Prisons FC

Filed in Michezo by on 19/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), Young Africans SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi hiyo leo Jumapili kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Tanzania Prisons iliyokuwa inaongozwa na Kocha Msaidizi na mchezaji wa zamani wa timu hiyo ilitangulia kwa bao la Samson Mangula kwa kichwa dakika ya 12 akimalizia mpira wa Kona wa Lambert Sabiyanka kutoka upande wa kushoto.

Kiungo Mzanzibari, Feisal Salum ‘Fei Toto’ akaisawazishia Yanga dakika ya 23 kwa shuti kali baada ya kazi nzuri ya kiungo Khalid Aucho ambaye yeye mwenyewe alifunga bao la ushindi dakika ya 43 kwa kichwa cha kuchupia mpira chini chini kufuatia krosi ya kiungo Saido Ntibazonkiza.

Kwa ushindi huo, Young Africans SC inafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa sasa na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao wamecheza mechi nane.

Hali ni mbaya kwa Tanzania Prisons inayobaki na pointi zake nane za mechi tisa katika nafasi ya 13 kwenye Ligi yenye timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.

Huu ni Msimamo wa NBC Premier League baada ya mechi moja ya iliyopigwa leo Jumapili December 19, 2021, Young Africans SC ikizidi kujikita kileleni mwa Msimamo.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.