Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia jana Januari 29 hadi lao Januari 30, 2023 Mangungu alipata kura 1311 na Kaluwa kura 1045 katika jumla ya kura halali 2356 huku kura 7 zikiharibika.

Walioshinda nafasi ya wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba katika uchaguzi uliofanyika jana Januari 29 na kumalizika leo Januari 30, 2023 ni!

1:Dkt. Seif Ramadhan Muba – kura 1636
2:Asha Baraka – kura 1564
3:CPA Issa Masoud Iddi – kura 1285
4:Rodney Chiduo – kura 1267
5:Seleman Harubu – kura 1250

Uchaguzi huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.