Nijuze Habari

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.

Filed in Michezo by on 10/06/2022 0 Comments

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.WADHAMINI Wakuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Benki ya NBC jana Alhamis ya June 09,2022 walilianika hadharani Kombe la Ubingwa wa Ligi hiyo msimu huu 2021/2022, ambao utafikia ukingoni baadae mwezi huu wa sita.

Nijuze Habari Application

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.WADHAMINI Wakuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Benki ya NBC jana Alhamis ya June 09,2022 walilianika hadharani Kombe la Ubingwa wa Ligi hiyo msimu huu 2021/2022, ambao utafikia ukingoni baadae mwezi huu wa sita.

NBC inayodhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu huu 2021/2022, imefanya tukio hilo Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam katika hafla maalum, ambayo ilihudhuriwa na maafisa wa Benki hiyo, Bodi ya Ligi ‘TPLB’, Wawakilishi wa Vilabu pamoja na Waandishi wa Habari.

Akizungumza katika hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa ‘TPLB’ Almas Kassongo amesema Kombe hilo la ubingwa ambalo lina muonekano wa tofauti, litakuwa rasmi kwa Bingwa wa kila msimu wa Ligi Kuu, kuanzia msimu huu 2021/2022.

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.Kassongo pia amesema kuwa Wadhamini Wakuu Benki ya NBC wamekubali kutengeneza Kombe Mbadala (Bandia) ambalo litabaki kwa kila Bingwa wa kila msimu, ili kutoa nafasi ya Kombe halisi kurudishwa kwa wahusika kwaajili ya Msimu mpya wa Ligi Kuu.

“Kila msimu Bingwa atakabidhiwa Kombe halisi katika hafla maalum ya kukabidhi, lakini baada ya hapo tutampatia Kombe Mbadala (Bandia) kwaajili ya kumbukumbu.”

“Huu umekua ni utaratibu wa Dunia nzima kufanya hivyo, kwa hiyo Kombe hili halisi litaendelea kubaki kama lililovyo na litakabidhiwa kwa kila Bingwa wa kila msimu kwa kupokezana, ama kwa Bingwa yuleyule kama atajirudia” amesema Almas Kassongo.

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.Aidha NBC imekiri kufurahishwa na mwenendo wa Ligi Kuu msimu huu wa 2021/2022, baada ya kuingia mkataba wa udhamini na Shirikisho la soka nchini TFF.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Waziri Barnabas, katika hafla maalum ya kuonyesha Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu 2021/22.

Barnabas amesema licha ya kuwa ndani ya mwaka wa kwanza wa udhamini wao, wameona mambo mengi yakiendeshwa kisasa na mwenendo wake unafurahisha, hivyo hawana budi kuzipongeza mamlaka ya soka na wadau wote wa mchezo huo nchini Tanzania.

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.“Tunashukuru sana kwa hapa tulipofikia, pongezi nyingi ziende ‘TFF’, Bodi ya Ligi ‘TPLB’ pamoja na wadau wengine wa mchezo wa soka nchini Tanzania, kwa namna mambo yanavyokwenda.”

MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.“Sisi tumeingia kwa mwaka wa kwanza katika udhamini, lakini tumefurahi sana kwa yote yanayoendelea katika Ligi Kuu, kwa hiyo nichukue nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Azam Media kama washirika wetu katika udhamini, tunashirikiana nao vizuri.”

“Nivishukuru vilabu kwa ushirikiano ambao tunaupata kutoka kwao, tunapata muonekano wa kutosha, waamuzi pia tunawashukuru sana popote walipo kwa kuonesha weledi wao, mashabiki wanaohudhuria katika michezo ya Ligi Kuu pamoja na Waandishi wa Habari kuiongelea vizuri Ligi yetu.”

“Ombi langu moja ni kwamba, sisi kama NBC bado tupo sana katika soka, tunamaliza hii sehemu ya kwanza, lakini bado tuna miaka mingine mbele na tutaendelea kuboresha zaidi udhamini katika zawadi na mambo mengine.” Amesema Barnabas

Wadhamini hao wa Ligi Kuu wametaja zawadi watakayotoa kwa Bingwa wa msimu huu, ambayo ni Sh. Milioni 100, maana yake Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu ataondoka na Sh. Milioni 600 jumla pamoja na Sh. Milioni 500 za haki ya matangazo ya Televisheni kutoka Azam Media Limited.

Huu hapa ni mgawanyo wa zawadi za fedha kulingana nafasi ya Klabu kwa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/2022.MGAWANYO wa zawadi za fedha kulingana nafasi kwa Ligi Kuu 2021/2022.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.