Nijuze Habari App

MIPANGO mitano muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya 2023

Filed in Makala by on 01/01/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

MIPANGO mitano muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya 2023

MIPANGO mitano muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya 2023

MIPANGO mitano muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya 2023

MIPANGO mitano muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya 2023, Kwa kawaida, Mwaka mpya unapowadia, watu hujiwekea maazimio na malengo mengi ya kutimiza katika mwaka huo.

Mara nyingi huwa ni kupunguza uzani, kufanya mazoezi zaidi, kuacha kuvuta sigara, kujifunza lugha mpya na kadhalika.

Lakini mara nyingi malengo haya huwa hayatimizwi.

Hatuwezi kukwambia ni maazimio gani unafaa kuyafanya, lakini kuna utafiti uliofanywa ambao unaweza kukuelekeza jinsi ya kujiwekea malengo ambayo utaweza kuyatimiza na pia njia bora zaidi ya kuhakikisha unatimiza malengo hayo.

Kuna ushahidi kwamba mara nyingi binadamu huongozwa na hamu ya “kupunguza hasara” – yaani, huwa mara nyingi tunaongozwa na kufuta hasara ambayo tumepata badala ya kupiga hatua mbele.

Kuweka maazimio kwa njia ambayo lengo lako zaidi litakuwa kupunguza au kufuta hasara, kwa maana ya kupata kitu ulichokipoteza, huenda yakawa rahisi kutimiza kuliko maazimio ya kukipata kitu kipya.

Mfano, inaweza kuwa rahisi kwako kuurejelea uraibu uliokuwa nao awali au kujiweka sawa kimwili kufikia kiwango cha awali kuliko kuboresha muonekano wako au uwezo wako kufikia viwango ambavyo haujawahi kuvifikia awali.

Hili pia linatuelekeza kwa ushauri mwingine muhimu unapojiwekea malengo yako ya mwaka – kabla lazima yawe ya uhalisia, yanaweza kutimizika.

Bila shaka kulikuwa na mafanikio, changamoto, makosa uliyoyafanya, uzoefu uliokufurahisha na uliokuza ujuzi wako, na mambo ambayo hayakukufurahisha katika mwaka huu…haya ni mambo ya kawaida ambayo hayapasi kukukatisha tamaa.

Andika mambo haya mahali ili uyatumie kuweka mkakati wako kuwa wa maana kwa ajili ya mwaka ujao.

Angalia mambo unayofaa kuyapa kipaumbele katika mipango yako ya mwaka.

Je ni mambo gani unayopaswa kuyaangalia unapoandaa mipango ya mwaka ujao? .

Angalia yale yaliyokuendeleza na yaliyokurudisha nyuma.

1.Tofautisha mipango yako ya kikazi na kibinafsi

Malengo yako ya kikazi yatakuwa ni tofauti na yale ya kibinafsi, licha ya kwamba yanategemeana. Vinginevyo huenda usifanikiwe kwa kiasi ambacho ulikitarajia.

2.Andaa mpango kwaajili ya mwaka mpya

Fikiria ni malengo gani hasa unayotaka kuyafikia tarehe 31 December ya mwaka ujao. Kisha, panga hatua unazohitaji ili uweze kuyafikia malengo hayo.

Andika mahali shughuli muhimu au mafanikio unayotarajia kuyaona kama viashiria vya vitakavyokuwezesha kufikia mafanikio hayo.

Viashiria hivi vinaweza kuwa miradi, au ujuzi wa kitaaluma.

Pia, angalia uwezekano wa vikwazo vya mafanikio uliyoyapanga.

Kama mwaka uliopita umetufundisha kitu fulani, hicho ndicho kitakacho kuwa mpango wa pili au wa tatu kama mambo hayatakwenda ulivyopanga.

Huenda usihitaji mipango hii mbadala.

Kuwa na mipango hii mbadala hata hivyo hutusaidia kuwa na kiasi fulani cha utulivu wa akili, huku tukijiandaa kusonga mbele na mpango wa awali.

3.Panga orodha ya mambo ambayo hautayafanya
Kupanga orodha ya mambo ambayo hautayafanya haimaanishi kuwa unaachana na mambo ambayo hutaki kuyafanya.

Ni pia kuachana na mambo ambayo yanakuzuia kiutendaji kufikia malengo yako.

Kubaini mambo ambayo unapaswa kuachana nayo itakuwezesha kuwa na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa malengo yako ya mwaka.

4:Tenga muda kwaajili yako binafsi.

Panga muda wako binafsi wa likizo au mapumziko mapema. Kama unahisi kuwa unahitaji kwenda kutembea mahala fulani, jipange mapema na utenge kiasi cha pesa zinazoweza kukuwezesha kwenda likizo.

Mchoko na msongo wa mawazo wa kuendelea kufanya kazi bila kupumzika sio mzuri kwa afya yako binafsi, na wala kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika hakukuongezei uwezo wa ufanisi wa kikazi kwaajili ya kufikia malengo yako.

Ni muhimu kufikiria kwa umakini afya ya mwili na akili yako, unapopanga malengo yako ya mwaka ujao.

5.Panga mradi wako wa kando ili ukuongezee kipato
Angalia kati ya mambo unayoyapenda uyatumie kama mradi wako wa kando wa kukuongezea kipato, usitegemee sana kazi unayoifanya pekee kama chanzo cha mapato yako.

Mradi wa kando hukusaidia kujifunza mbinu mpya na ujuzi ambao vinginevyo

Usingeupata katika kazi yako ya kila siku, na unaweza kukunufaisha kimaisha.

Kila mara uwe na subra na furahia kila kitu unachojifunza.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Washirikishe wengine
Mwanafalsafa katika Chuo Kikuu cha Warwick Dkt John Michael hutafiti kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii yanayowasaidia watu kutimiza malengo na ahadi zao.

Anasema kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kutimiza ahadi na maazimio iwapo tutayatazama kwamba yana umuhimu kwa watu wengine – kwamba maslahi ya wengine yatakuwa hatarini iwapo tutashindwa.

Hii huenda ikawa ni kwenda darasani na rafiki yao.

Ufanisi unaweza kuwa hata zaidi iwapo utalipa karo mapema – ukihisi kwamba mtu amewekeza pesa na muda wake, na kwamba vyote vitapotea, basi kuna uwezekano kwamba utajizatiti kutimiza malengo hayo.

Utafiti wa Dkt Michael pia unaonesha kuwa watu huenda wakahamasishwa kuendelea na kazi wasiyoipenda iwapo mtu mwingine wa maana kwao amewekeza kitu hapo.

Vitu vya kukukumbusha
Sifa na hadhi ya mtu huwa muhimu sana, na vinaweza kutumika kama kichocheo.

Kuyafanya maazimio yako wazi kunaweza kukuhamasisha kuyatimiza kwani utahofia kwamba hadhi yako itashuka iwapo hutayatimiza.

“Huwa hakuna anayetaka kupata sifa za kuwa mtu asiyeaminika, kwa hivyo hutangaza mipango yetu hadharani kunaweza kutupatia motisha.

Kuweka dau kunaweza pia kuwa kichocheo zaidi,” anasema Prof Neil Levy wa Chuo Kikuu cha Oxford.

Kuweka maelezo zaidi na ufafanuzi kwenye maazimio yako pia husaidia, anasema.

Mfano kwenda kwenye chumba cha mazoezi Jumanne alasiri na Jumamosi asubuhi, kwa mfano, ni bora kuliko kusema tu kwamba utaenda kufanya mazoezi mara nyingi zaidi, anasema Prof Levy.

Anapendekeza uhusishe maazimio yako na viashiria au vitu fulani vya kukukumbusha.

Kisha, ndipo ujiwekee nafasi ya kufanikiwa zaidi, unaweza kuweka ujumbe wa kukukumbusha kufanya hivyo kwenye kidhibiti mweleko wa gari kila jioni kabla ya kulala.

Hapo, unaeleza nia na pia kuchukua hatua kuhakikisha unaitekeleza nia hiyo.

Kuweka masharti
Prof Levy anaonya pia dhidi ya kujiwekea masharti ambayo yanaweza kuwa vielelezo baadaye.

“Kubali wazi kwamba kuna baadhi ya mambo yanayoweza kukuzuia kufanya jambo (Sitakwenda kwa mazoezi iwapo nyumba itashika moto). Lakini usipanue masharti haya au kuyafanya kuwa mtindo kwani yanaweza kukuzuia kutekeleza maazimio yako.

“Siku yangu ya kuzaliwa, inaweza kuwa siku ya kipekee na inakubalika. Lakini nikianza kutambua mambo yanayofanyika mara kwa mara – pengine iwapo ni wiki ya mwisho ya mwezi, kuwepo kwa baridi kali – basi itakuwa mazoea,” anasema.

Kufanya maazimio kuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu
Kwa Dkt Anne Swinbourne, mwanasaikolojia katika chuo kikuu cha James Cook, Australia, maazimio bora zaidi ni yale ambayo yanaoana na malengo ya muda mrefu ambayo umejiwekea wewe binafsi, kuliko yale ambayo hayana msingi au ni matamanio tu.

Iwapo hujawahi kuonesha nia ya kushiriki katika michezo, kujiwekea malengo ya kuwa mwanariadha stadi ni lengo ambalo bila shaka utatatizika kutimiza.

Kwa sababu umekua na ndoto ya muda mrefu ya kusafiri sana kujionea ulimwengu kabla ya kutimiza miaka 50, lengo la kusafiri zaidi linaweza kutimizika.

Tambua ni mambo gani anakuchochea kufanya mambo usiyoyapenda. Iwapo hutaki kunywa pombe sana, panga kukutana na marafiki au wageni wako kwenye mgahawa badala ya baa, vilevile, ukipanda kuacha kuvuta sigara, vyema zaidi ni kuacha kujihusisha na wavutaji sigara sana.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

DONWLOAD HAPA SISI kwetu Michezo ndo Furaha yetu.

Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari za Michezo, Nijuze Habari, Nijuze Michezo, Nijuze TV App, Nijuze TV LIVE, Nijuze Habari Michezo, Nijuze Habari Magazeti, Nijuze Habari Ajira, Nijuze Habari Usajili, Nijuze Habari Matokeo, Nijuze Habari Usajili, saleh jembe michezo leo,habari za michezo
leo 2023, habari za yanga za leo, habari za simba za leo, Habari za Michezo leo 2023.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *