telegram Nijuze Habari

Mo Dewji atoa billion 2 ujenzi Uwanja wa Simba

Filed in Michezo by on 13/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Mohamed Dewji ‘Mo’ amehahidi kutoa TSh2 billion kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wao mpya.

Simba inamiliki uwanja wa mazoezi Simba Mo Arena uliopo Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambao ulipunguza matumizi makubwa ya Pesa ambazo walikuwa wakizitumia kukodi viwanja vya mazoezi.

Simba ilikuwa ikilipa kila siku sh 500,000 katika viwanja ambavyo walikuwa wakipenda kuvitumia kwaajili ya mazoezi yao gharama ambazo kwa sasa zinafanya majukumu mengine.

Kupitia kurasa zake za kijamii hii leo, Mo Dewji ameandika kuwa yuko tayari kuchangia kiasi hicho cha Pesa kwaajili ya ujenzi huo huku akiwataka wanasimba kumuunga mkono katika harakati hizo.

Amesema, amefikia hatua hiyo baada ya kupokea maombi mengi ya wanasimba juu ya uhitaji wa kuwa na Uwanja wao binafsi.

“Nimepokea maoni mengi ya wanasimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu, na wako tayari kuchangia ili tunafinikishe ujenzi huo, naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni yao kwa mikono miwili,”ameandika Mo katika kurasa zake za Twitter na Instagram.

“Naomba bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji, kwa kuanza nahaidi kuchangia tsh 2 billion nawaomba wanasimba tuchangie sote,”ameandika Mo.

Wakati Mo ameingia Simba kama Mwekezaji alionyesha nia ya kujenga Uwanja ambapo hivi sasa klabu hiyo inautumia kwaajili ya mechi za kirafiki na mazoezi yao ya kila siku.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *