Morrison arejea Simba

Filed in Michezo by on 14/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

Klabu ya Simba yamrejesha Kikosini Winga Mghana, Benard Morrison ‘BM3

Benard Morrison, Simba SC, BM3, Simba, Barbara Gonzalez, Benard Morrison Simba SC.

KLABU ya Simba SC imethibitisha kuwa winga Bernard Morrison raia wa Ghana amerejeshwa kikosini Jumatatu February 14,2022 baada ya kumaliza kesi ya utovu wa nidhamu iliyokuwa ikimkabili.

Taarifa iliyotolewa na Simba, imebainisha kuwa Morrison aliomba radhi kwa Uongozi na Wachezaji wenzake na leo aliweza kuonana na CEO wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez ambapo baada ya mazungumzo aliruhusiwa kurejea kikosini.

Morrison tayari ameungana wenzake mazoezini kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Ruvu Shooting, Mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa Jumatano ya Februari 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Katika kipindi ambacho Morrison alikuwa amesimamishwa alikosa michezo mitatu dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya Kwanza na wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Asec Mimosas ambao Simba walishinda 3-1.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *