Nijuze Habari

Morrison ashinda Kesi vs Yanga SC

Filed in Michezo, Usajili by on 22/11/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MAHAKAMA ya usuluhishi wa kesi za michezo Duniani (CAS) imetupilia mbali rufaa ya Klabu ya Young Africans SC ya kupinga uamuzi uliotolewa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuwa mchezaji wa kimataifa wa Ghana, Bernard Morrison hakuwa na mkataba nao kipindi anajiunga na Simba.

Young Africans SC ilipinga uamuzi wa kamati hiyo ya TFF uliotolewa August, 12, 2020 ambao ulikuwa ukieleza kwamba Morrison hakusaini nao mkataba ingawa ilithibitika kwamba Yanga ilimpa Dola 30,000 ambazo kamati ilimuamuru mchezaji huyo airudishie Yanga Pesa hiyo.

Kamati hiyo ilidai mkataba wa Morrison na Young Africans SC ulimalizika July 14, 2020, hivyo kuanzia hapo alikuwa huru na mkataba wa mara ya pili wa Yanga haukuwa unatambulika rasmi.

Baada ya Young Africans SC kupinga uamuzi huo wa TFF ilikata rufaa kwenda CAS ikiomba uhalali wa mkataba waliodai kuwa wamemsainisha kwa mara yapili na Morrison aamrishwe kulipa Dola 200,000 kama adhabu ya kusaini mkataba na Klabu nyingine ya Simba SC wakati bado alikuwa na mkataba na Young Africans SC.

Baada ya rufaa hiyo CAS kupitia taarifa yake iliyotoa leo imefafanua kwamba ilikaa kikao kwa njia ya video July mwaka huu na baada ya majadiliano imefikia uamuzi wa kuitulipilia mbali rufaa hiyo iliyowasilishwa na Young Africans SC.

Baada ya kushinda Kesi hiyo, Mchezaji Benard Morrison ametakiwa kulipwa kitita cha Swis 5,000 (sawa na Sh12,396,787) na Klabu ya Young Africans.

Morrison alisajiliwa na Young Africans SC kwenye dirisha dogo la Usajili  Msimu wa 2019/2020, ambapo aliitumikia Klabu hiyo kwa miezi kadhaa kabla ya kutimkia Simba SC.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.