Nijuze Habari

MORRISON Asimulia sakata la kuondolewa Simba, Ugomvi na CEO, Try Again -Video

Filed in Usajili by on 30/06/2022 0 Comments

MTANDAO wa GLOBAL TV umefanya mahojiano maalum na mchezaji Benard Morrison, kuhusiana na masuala mbalimbali yanayomhusu, ikiwemo sababu za kuondoka Simba na klabu anayoelekea.

Nijuze Habari Application

MORRISON Asimulia Sakata la kuondolewa Simba, Ugomvi na CEO, Try Again -VideoMORRISON Asimulia Sakata la kuondolewa Simba, Ugomvi na CEO, Try Again -Video

MTANDAO wa GLOBAL TV umefanya mahojiano maalum na mchezaji Benard Morrison, kuhusiana na masuala mbalimbali yanayomhusu, ikiwemo sababu za kuondoka Simba na klabu anayoelekea.

Morrison amesema “Walinipa mapumziko maana nilikataa kusaini mkataba mpya, kama ningecheza Simba miaka 5 au 10 halafu mwisho wa siku nikarudi Ghana sina hela au kumpigia mwenyekiti naomba hela kuisaidia familia yangu isingekuwa kitu kizuri.

“Niliomba mkataba mzuri, maboresho kwenye mkataba ili niwe vizuri kuihudumia klabu na haikufanyika hivyo, nilikuwa na kikao na Barbara na sababu ya hicho kikao ni kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga na ile mechi nilipata majeraha na awali tayari nilikuwa majeruhi kwenye mechi dhidi ya Orlando Pirates.

“Baada ya mechi daktari hakunifuata kunihudumia wala kujua hali yangu, nilimtumia meseji nyingi kuwa sipo sawa lakini hakufanya hivyo, niliwaambia hamnijali hivyo nililazimika kujihudumia mwenyewe nikiwa nyumbani.

“CEO alinipigia simu nikaenda ofisini kwake akaniambia wachezaji wanahasira, wanasema hawataki niende tena kambini wala mazoezini, kocha analalamika siwaheshimu, hawataki niende mazoezini hivyo malalamiko ni mengi ni kwa nini nafanya hivyo?

“Nilimjibu sio kweli sidhani kama wachezaji wanaweza kufanya hivyo maana ndio haohao wachezaji wananipigia simu nisipoonekana kambini kunijulia hali lakini wewe CEO unasema hivi.

“Kocha alinipigia simu tukaongea kama dakika 40 nikamuuliza baada ya mkutano wangu na CEO unadhani kuna nini kitatokea akanijibu hadhani kama kuna namna ya mimi kurudi klabuni na kwa vile CEO aliniambia nenda ukakae nyumbani usubiri nitakupigia nikajua kuna jambo linaendelea.

“Asubuhi yake nilimpigia CEO akaniambia niende ofisini kwake, nilipoenda akaniambia mambo mawili, la kwanza nikubali kwenda nyumbani nikae nje ya klabu hadi mwisho wa msimu halafu watawaambia mashabiki nimeenda nyumbani kwa matatizo ya kifamilia na nitarudi mambo yakiwa sawa au ataweka kwenye social media kuwa wamenisimamisha hadi mwisho wa msimu,” amesema Morrison katika sehemu ya mahojiano hayo.

Credit: Global Publishers

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

DOWNLOAD APP MPYA YA NIJUZE HABARI BURE HAPA

UPATE KUTAZAMA MECHI LIVE, MAGAZETI YA KILA SIKU ASUBUHI PAMOJA NA HABARI NYINGINE NYINGI.

TEMBEA NA DUNIA MKONONI MWAKO UKIWA NA APP HII, FURAHIA HABARI NA MATUKIO KILA WAKATI.

Download Bure App mpya ya Nijuze Habari kuweza kuangalia Mpira na utaweza kuona matokeo na ratiba ligi zote kubwa Duniani.

APP HII PIA INAKUSOGEZEA

👉HABARI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA
👉HABARI ZA MICHEZO NA USAJILI
👉BREAKING NEWS
👉ELIMU NA AFYA
👉KUTAZAMA MECHI MUBASHARA
👉TAARIFA YA HABARI NA VIPINDI MBALIMBALI
👉KUSIKILIZA RADIO ONLINE
👉KUCHECK MOVIE (KIX CHANNEL, MAISHA MAGIC BONGO, MAISHA MAGIC EAST N.K)
👉 KUCHECK MIELEKA (WWE)
👉MAPENZI NA MAHUSIANO
👉AUDIO MPYA KILA SIKU
👉 AJIRA MPYA KILA SIKU
👉GOSPEL
👉MAKALA.

BOFYA 👉👉👉 HAPA KUDOWNLOAD BURE

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.