telegram Nijuze Habari

Morrison mchezaji bora Simba SC

Filed in Michezo by on 02/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KIUNGO machachari wa Simba SC raia wa Ghana, Bernard Morrison ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki ya mwezi November (Emirates Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month).

Morrison ametajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo akiwashinda Mshambuliaji kutoka Rwanda Meddie Kagere na Kiungo wa Mtanzania Jonas Mkude.

Morrison aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi November huku akiisaidia Simba SC kuibuka mshindi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Mshambuliaji Meddie Kagere aliingia kwenye mchakato wa kumsaka mshindi wa mwezi November, kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao akiwa na kikosi cha Simba kwa mwezi November, ambapo alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC, Ruvu Shooting na Red Arrows.

Upande wa Mkude amekuwa muhimili mkubwa katika safu ya kiungo tangu alipokabidhiwa jukumu hilo, baada ya kuondoka kwa Kocha Didier Gomes, mwezi November alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC, Ruvu Shooting na Geita Gold huku akisimama imara kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Aidha tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki kwa mwezi October (Emirates Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month), ilichukuliwa na Kiungo Mshambuliaji Hassan Dilunga ‘HD’.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *