telegram Nijuze Habari

Nabi ratiba yetu ni ngumu, watatu kuikosa Kagera Sugar

Filed in Michezo by on 12/11/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

Nabi ratiba yetu ni ngumu, watatu kuikosa Kagera Sugar, wanne waongeza nguvu

Kagera Sugar FC vs Yanga, Matokeo Kagera Sugar vs Yanga SC 13 November 2022, Matokeo Yanga SC vs Kagera Sugar FC NBC Premier League 2022/2023, Matokeo Yanga vs Kagera Sugar FC 13 Nov 2022, Young Africans SC vs Kagera Sugar 12 November 2022, Magoli waliyofunga Yanga vs Kagera Sugar, Msimamo wa Ligi.

NABI ratiba yetu ni ngumu, watatu kuikosa Kagera Sugar

NABI ratiba yetu ni ngumu, watatu kuikosa Kagera Sugar

KUELEKEA mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar, Benchi letu la ufundi la Young Africans limefanya mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza.

Akiongoza Mkutano huo, Kocha Mkuu Nasreddine Nabi na Msaidizi wake Cedric Kaze pamoja na Mshambuliaji Yusuf Athumani walijibu maswali ya waandishi wa habari waliokusanyika kwenye makao makuu ya benki ya NBC iliyopo Jijini Mwanza.

MATOKEO Yanga vs Kagera Sugar 13 November 2022

“Ratiba yetu ni ngumu sana. Tumemaliza muda mwingi kwenye ndege kuliko uwanja wa mazoezi. Tangu jumatano hatujafanya mazoezi kujiandaa na mchezo huu.

“Tumefika Mwanza jana usiku na tuna siku moja tu ya mazoezi. Hii sio rafiki kwa afya ya mwili wa wachezaji.

Hatuko hapa kulalamika lakini tunaamini viongozi wa mpira wetu jambo hili kwa wakati mwingine wanatakiwa kulitazama kwa jicho tofauti. Tulikwenda Tunisia kuiwakilisha Tanzania,” alisema Nabi

“Kiakili wachezaji wetu wako vizuri, kwa sasa tunashirikiana kwa karibu na jopo letu la madaktari kujua utimamu wa mwili wa wachezaji wetu kabla ya mazoezi ya leo jioni.

“Kucheza Yanga ni kujitoa na huu ni wakati ambao wachezaji wetu wanatakiwa kujitoa sana kwaajili ya timu yao. Wamekosa muda wa kupumzika na wanajua wamekuja Mwanza kupambana.

“Kagera ni wapinzani wagumu, tunawaheshimu sana lakini tunaamini wachezaji wetu watajitoa kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri, aliongeza kocha Nabi.NABI ratiba yetu ni ngumu watatu kuikosa Kagera Sugar

KIKOSI Cha Yanga vs Kagera Sugar 13 November 2022

“ Ni kweli Aziz Ki atakosekana. Amefungiwa na Bodi ya Ligi na sisi benchi la ufundi tumemruhusu akajiunge na kambi yake ya timu ya Taifa.

“Tunaamini huko atakuwa kwenye maandalizi mazuri ya kucheza na atarudi akiwa imara sana.
“Aziz ni mchezaji mkubwa lakini Yanga haijajengwa kwa kumtegemea mchezaji mmoja. Hii ni timu na kila mmoja anatakiwa kutoa mchango wake kuisaidia timu.

“Falsafa yetu inatusaidia kucheza hata tunapokosa mchezaji mmoja basi madhara yasiionekane.”

“Tunasubiri ripoti ya daktari kuhusu afya ya Aucho na ya wachezaji wengine. Kwenye mazoezi ya leo tutaona nini tutafanya kiufundi kuelekea kwenye mchezo wa kesho.

“Lakini kwa Aucho sio kwamba tulimtoa kwa sababu alipata majeraha makubwa. Nafikiri mliona alipata kadi na tukawa na hofu kwa mazingira ya mechi yalivyokuwa angeweza kupata kadi nyingine na mzigo ukawa mzito kwa timu,” aliongeza Nabi.

Aidha beki wa kulia wa Young Africans, Djuma Shaban raia wa DR Congo ni miongoni mwa Wachezaji 22 walisafiri kwenda Mwanza kwaajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar.

Djuma aliikosa safari ya Tunisia kwa sababu za jeraha za nyama za paja, ameongezwa kwenye safari ya Mwanza, pamoja na kinda Dennis Nkane, Yusuf Athumani na kinda kutoka U 20, Clement Mzize

Wachezaji waliokosekana kwenye safari hii ya Mwanza ambao wataukosa mchezo huo ni Heritier Makambo aliyepata jeraha la kidole cha mguu kwenye mazoezi, nchini Tunisia.

Nyota wengine wanaokosa safari ni Gael Bigirimana aliyeondoka nchini kwenda Burundi kujiunga na timu yake ya Taifa, Kiungo Stephane Aziz Ki anayetumia adhabu ya kufungiwa mechi 3 na Bodi ya Ligi.

Licha ya adhabu hiyo, Aziz KI amejiunga na timu yake ya Taifa ya Burkina Faso inayotarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ivory Coast, November 19, 2022.

Sambamba na hilo Kampuni Bora ya kubet Tanzania SOKABET inakukaribisha kuweka bashiri zako katika Michezo Mbalimbali kama LIVE Casino, Slots, Zeppelin, Virtual Game, Basketball na Mpira wa Miguu.

Faida ya kuweka bashiri zako kupitia SOKABET ni upatikanaji wa Bonusi za Viwango, kama 100% kwa wekezo la kwanza, 10% kwa Casino na Mpira wa Miguu Pamoja na Multibonus hadi 750.

Sehemu pekee ya kupiga pesa kiurahisi na kufanya miamala kwa haraka zaidi ni SOKABET the best sports Betting in Tanzania.

Aidha Nijuze Habari Kupitia nijuzehabari.co.tz tutakuleta moja kwa moja Matokeo ya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumapili ya November 13,2022 kuanzia saa 10:00 Jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.

Pamoja na Matokeo pia Nijuze Habari itakuletea Kikosi Cha Young Africans Kinachoanza dhidi ya Kagera Sugar FC mapema iwezekanavyo.

KUONA Kikosi Cha Yanga SC kinachoanza vs Kagera Sugar Bofya HAPA

LIVE Kagera Sugar FC vs Yanga SC November 13 2022

KUONA Matokeo ya Mchezo huo Kati ya Kagera Sugar vs Young Africans Bofya HAPA.

Yanga vs Kagera Sugar Mechi walizokutana, Head to head Yanga vs Kagera Sugar, Yanga vs Kagera Sugar CCM Kirumba.Yanga SC vs Kagera Sugar, Matokeo ya Yanga vs Kagera Sugar, Matokeo Yanga vs Kagera Sugar leo, Matokeo Kagera Sugar vs Yanga leo, LIVE Yanga SC Kagera Sugar, Live Yanga vs Kagera Sugar 13 November 2022, Yanga vs Kagera Sugar, Kagera vs Yanga.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *