NABI tuko tayari vs Malumo Gallants, aomba jambo kwa Mashabiki

Filed in Michezo by on 09/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

NABI tuko tayari vs Malumo Gallants, aomba jambo kwa Mashabiki

NABI tuko tayari vs Malumo Gallants, aomba jambo kwa Mashabiki

NABI tuko tayari vs Malumo Gallants, aomba jambo kwa Mashabiki

KOCHA Mkuu wa Klabu Young Africans, Nasreddine Nabi amesema kuwa Marumo ni timu nzuri na wamejiandaa kukabiliana nao kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Nabi alisema kuwa watachuana na Marumo iliyotinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho na sio Marumo inayoshika nafasi za chini kwenye Msimamo Ligi kuu ya Afrika Kusini.

“Marumo ni timu nzuri, sisi tumejiandaa kucheza na timu iliyofika Nusu Fainali na sio nafasi yao kwenye Msimamo wa Ligi ya kwao”

Nabi pia amesema kuwa wanatambua hawawezi kufuzu Fainali kwa dakika 90 za mchezo wa kwanza nyumbani hapo kesho, wamejiandaa kwaajili ya kupambana kwa dakika 180 za mechi zote mbili.

“Ni mechi inayohitaji akili na tahadhari kubwa sana. Tunacheza mechi ya kwanza nyumbani lakini tunatambua hatuwezi kufuzu kwa matokeo ya mchezo mmoja. Tutacheza huku tukifahamu tuna dakika 180 za kufuzu”

“Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo, ari ya timu ni kubwa kila mchezaji akitamani kuwa sehemu ya mechi hiyo,” alisema Nabi

Mtunisia huyo amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwaongezea wachezaji wao hamasa ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Niwashukuru sana Mashabiki wa Yanga kwa sapoti mliyotupa kutoka mwanzo mpaka leo, nawaomba kesho tuongeze kitu kimoja. Kesho tushangilie kwa dakika zote 90, hata katika nyakati timu haina mpira tusiwe kimya, tupambane kushangilia ili kuwapa nguvu wachezaji wetu. Hii mechi sio nyepesi kama wengi wanavyodhani”

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *