NAFASI 45 za Kazi Manispaa ya Sumbawanga Leo April 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


NAFASI 45 za Kazi Manispaa ya Sumbawanga Leo April 2023

NAFASI 45 za Kazi Manispaa ya Sumbawanga Leo April 2023
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imepokea kibali cha Ajira mpya kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye kumb. Na. FA.97/228/01″ TEMP”06 cha tarehe 06.04.2023.
Kufuata idhini hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kutuma maombi ya nafasi hizo kwa kuzingatia sifa, vigezo, na maelekezo yaliyo katika tangazo hili.
1.MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VE III)- Nafasi 20
KAZI NA MAJUKUMU.
- Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mpango ya Maendeleo ya Kijiji.
- Kusimamia ulinzi na usalama wa rai ana mali zao.
- Kukusanya mapato ya Halmashauri ya Kijiji.
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote za nyaraka za Kijiji.
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji.
- Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kupokea na kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi Kazi nyingine atakazopangiwa na mwajiri.
SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne au sita pia awe amehitimu mafunzo ya Cheti/Astashahada katika moja ya fani, zifuatazo:
- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
ANGALIZO: Astashahada/Cheti kiwe na ngazi ya NTA – LEVEL 5)
- Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
2.MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (ME III) – Nafasi 25
KAZI NA MAJUKUMU
- Mratibu na Mtekelezaji wa sera na sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika
Mtaa. - Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu mipango ya Maendeleo katika Mtaa.
- Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umasikini katika Mtaa.
- Kusimamia Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu zawalipa kodi wote.
- Kuandaa na kutunza rejesta ya wafanyakazi wote wa Mtaa.
- Kusimamia utungaji na utekelekazaji wa sheria ndogo ndogo za mitaa.
SIFA ZA MWOMBAJI.
Cheti cha Kidato cha IV au VI
Aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:
- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
- Awe hajawahi kuajiriwa Serikalini.
(ANGALIZO: Astashahada/Cheti kiwe na ngazi ya NTA – LEVEL 5)
- Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
3.MAMBO YA KUZINGATIWA KWA WAOMBAJI.
- Muombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
- Awe mwenye umri kati ya 18-45
- Barua za muombaji ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, Taaluma, Cheti cha kuzaliwa na Picha mbili (2) za rangi (Passport size) za hivi karibuni.
- Maombi ya kazi yaambatanishwe na nakala ya Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA.
- Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi ya muombaji (CV)
- Testmonials “Provisional Result” Statement of Result” hati za matokeo za kidato cha nne na sita (Form IV and Form VI Results Slips) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi waambatanishe uthibitisho wa vyeti vyao kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI:-
Barua ya maombi iandikwe kwa mkono na iambatanishwe na passport size mbili (2).
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 08/05/2023 saa 9:30 Alasiri
Maombi yote yatumwe kwa Anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga,
S.L.P 187, SUMBAWANGA
NAFASI 45 za Kazi Manispaa ya Sumbawanga Leo April 2023, Sumbawanga Municipal Council address,Jina la mkuu wa wilaya ya sumbawanga,Historia ya wilaya ya sumbawanga,Ramani ya sumbawanga,Dew Drop water sumbawanga jobs,Vijiji vya sumbawanga.
UNAWEZA PIA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Dew Drop water sumbawanga jobs, Historia ya wilaya ya sumbawanga, Jina la mkuu wa wilaya ya sumbawanga, NAFASI 45 za Kazi Manispaa ya Sumbawanga Leo April 2023, Ramani ya sumbawanga, Sumbawanga Municipal Council address, Vijiji vya sumbawanga.