NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha May 2023

Filed in Ajira by on 26/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha May 2023

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha May 2023,Wilaya za Arusha,1Kata za wilaya ya arusha vijijini,Arusha District Council address,Kata za arusha dc,Majina ya mitaa ya arusha mjini,Mkuu wa wilaya ya arusha mjini 2023,Arusha District Council Job Vacancies May 2023,arushadc.go.tz, Nafasi za kazi Halmashauri ya jiji la Arusha Tanzania|Latest job,Nafasi za kazi Halmashauri ya jiji la Arusha - Arusha City Council,Arusha District Council,Jobs in Arusha, Vacancies Offers - May 2023.

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha May 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha amepokea kibali cha kutekeleza Ikama na Bajeti kwa Ajira Mpya kwa mwaka wa fedha 2022/2023 chenye Kumb.Na.FA.971/288/01/’TEMP/06 cha tarehe 06 April, 2022 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha anawatangazia wananchi wote ambao ni Raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapa chini: –

1:DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2 – TGS B

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe amefaulu kidato cha nne (iv) au cha sita (vi).
  • Leseni ya daraja E au C ya Uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
  • Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la Il watafikiriwa kwanza.

MAJUKUMU YA KAZI YA UDEREVA:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari na Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelezwa na Msimamizi wa kazi.

2:MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA III (NAFASI 2):

SIFA ZA MWOMBAJI:

  • Awe amefaulu kidato cha nne (IV)
  • Awe amehudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu ngazi ya Stashahada (Diploma) kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe amefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza, maneno yasiyopungua 80 kwa dakika moja.
  • Awe na cheti cha programu ya windows, Microsoft office, Internat-E-mail na Publisher, Power point kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA III

  • Kuchapa barua taarifa na nyaraka za kawaida na SIRI.
  • Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikia.
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wako na ratiba ya kazi nyingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika
    Idara/Kitengo/Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya Vikao mbalimbali.
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

MASHARTI YA UJUMLA:

  • Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
  • Mwombaji aambatanishe nakala ya kadi ya NIDA
  • Mwombaji aambatanishe cheti cha kuzaliwa
  • Mwombaji aambatanishe maelezo yake binafsi (CV) pamoja na hamba za simu zinazopatikana muda wote
    Mwombaji awe na wadhamini watatu na namba za simu ambazo zinazopatikana muda wote
  • Mwombaji wakati wa kuwasilisha maombi aweke picha ndogo (Passport size) moja iliyoandikwa jina kwa nyuma na ibandikwe kwenye barua ya maombi.
  • Barua ziandikwe kwa mkono na ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu pamoja na taaluma.
  • Testimonial, Provisional result, statement of result HAVIKUBALIKI
  • Waombaji wote ambao wamesoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimefanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE na kuambatanisha taarifa kutoka Mamlaka husika.
  • Madereva waambatanishe maombi la Leseni ya udereva.
  • Waombaji wote watatakiwa kuangalia mara kwa mara kwenye tovuti wa Halmashauri kwa sababu watakaoitwa kwenye usaili wa awali majina yao yatawekwa kwenye tovuti ya Halmashauri ambayo ni www.arushadc.go.tz

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06.06.2023.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili “HAYATAFIKIRIWA”.

MAOMBI YOTE YATUMWE KWA NJIA YA POSTA KATIKA ANUANI IFUATAYO:

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA,
S.L.P 2330,
ARUSHA.
449
MKURUGENZI MTENDAJI ARUSHA HALMASHAURI YA WILAYA ARUSHA
Seleman H. Msumi MKURUGENZI MTENDAJI (W)
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, S.L.P. 2330, Mkoa wa Arusha, Simu 073 6500476 nukushi 2503701, Barua pepe ded@arushadc.go.tz, Tovuti. www.arushadc.go.tz

Wilaya za Arusha,1Kata za wilaya ya arusha vijijini,Arusha District Council address,Kata za arusha dc,Majina ya mitaa ya arusha mjini,Mkuu wa wilaya ya arusha mjini 2023,Arusha District Council Job Vacancies May 2023,arushadc.go.tz, Nafasi za kazi Halmashauri ya jiji la Arusha Tanzania|Latest job,Nafasi za kazi Halmashauri ya jiji la Arusha – Arusha City Council,Arusha District Council,Jobs in Arusha, Vacancies Offers – May 2023.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *