NAFASI za Kazi Manispaa ya Kinondoni May 2023

Filed in Ajira by on 03/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

NAFASI za Kazi Manispaa ya Kinondoni May 2023

NAFASI za Kazi Manispaa ya Kinondoni May 2023,Ofisi za manispaa ya kinondoni,Kata za manispaa ya kinondoni,Mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni,Manispaa ya kinondoni address,WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

NAFASI za Kazi Manispaa ya Kinondoni May 2023,Ofisi za manispaa ya kinondoni,Kata za manispaa ya kinondoni,Mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni,Manispaa ya kinondoni address,WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

NAFASI za Kazi Manispaa ya Kinondoni May 2023

Kufuatia Serikali kutoa idhini ya Utekelezaji wa Ikama na Bajeti kwa Ajira Mpya katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, kwa Kibali chenye Kumb. Na. FA.97/228/01 “TEMP”/06 cha Tarehe 06 Aprili, 2023, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatangaza nafasi ya Ajira kwa Kada ya Madereva kwa Watanzania wenye sifa kama ilivyoainishwa hapa chini:-

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI MBILI (2)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form Four) na Leseni ya Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua Mwaka Mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) au Chuo kingine. Waombaji wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la Il watafikiriwa kwanza.

KAZI/MAJUKUMU YA KUFANYA

 • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
 • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
 • Kufanya Matengenezo madogomadogo ya gari
 • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
 • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
 • Kufanya Usafi wa gari na
 • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

WALIOITWA Kwenye Mafunzo ya awali ya Uchunguzi PCCB 2023

MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara wa Serikali TGS.B.1

NB: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI:-

 • Waombaji wote wawe raia wa Tanzania ambao hawazidi umri zaidi ya miaka 45 na hawapungui umri wa miaka 18,
 • Waombaji wote lazima waambatanishe wasifu binafsi (CV) wenye mawasiliano ya uhakika, anuani, barua pepe na namba za simu.
 • Waombaji wote waombe kwa kufuata masharti ya TANGAZO LA KAZI.
 • Waombaji lazima waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo
  a) Cheti cha Msingi cha Uendeshaji Magari kulingana na sifa za nafasi husika. b) Cheti cha mtihani wa kidao cha nne au sita,
  c) Cheti cha kuzaliwa.
  d) Nakala ya Kitambulisho cha Uraia (NIDA)
 • Hati ya matokeo ya kidato cha nne (Result slip) haitafanyiwa kazi.
 • “Transcript” ambayo haikuambatanishwa na cheti haitafanyiwa kazi.
 • Kuwasilisha vyeti vya kughushi na maelezo mengine itasababisha kuchukuliwa hatua za kisheria.
 • Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
 • Waombaji ambao walistaafu kazi kwa sababu yoyote ile hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
 • Waombaji waonyeshe wadhamini wawili na mawasiliano yao, anuani na namba za
  simu.
 • Waombaji wenye vyeti ambavyo vimepatikana nje ya nchi wahakikishe vimehakikiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Elimu ya ufundi la Taifa (NACTE) na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
 • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au kiingereza.
 • Watakaochaguliwa kufanya usaili watajulishwa tarehe ya usaili kupitia tovuti ya Halmashauri – www.kinondonimc.go.tz

FAHAMU Jinsi ya kupata namba ya NIDA (NIN)

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 07 Mei, 2023 saa tisa na nusu (9:30) Alasiri.

Maombi yatakayoletwa kwa mkono hayatapokelewa na hayatafanyiwa kazi

Maombi yote yatumwe kwa Anuani ainishwa hapa chini na si vinginevyo:-

Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,
S.L.P. 31902,
DAR ES SALAAM.
Hanifa S. Hamza
MKURUGENZI WA MANISPAA

Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, S.L.P. 31902, 2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam, Unaweza pla kuwasiliana nasi kwa Simu: +255 2170173 Nukushi: 2172606, Barua pepe- hr@kinondonimc.go.tz

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *