NAFASI za Kazi Mbeya Distric May 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


NAFASI za Kazi Mbeya Distric May 2023

NAFASI za Kazi Mbeya Distric May 2023
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anapenda kuwatangazia Watanzania Wote kuwa amepokea kibali cha Ajira Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.170/364/01″B”/52 cha 13/02/2023 kwaajili ya kujaza nafasi ya kazi ya Mtendaji wa Kijiji III na Dereva II ya Ajira ya Kudumu na Kibali cha Ajira mpya chenye Kumb.Na.FA.97/228/01.TEMP/06 cha tarehe 06.04.2023 kwaajili ya ajira mpya nafasi ya kazi ya Katibu Mahsusi III na Msaidizi wa Kumbukumbu II ya Ajira ya Kudumu.
DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2
KAZI ZA KUFANYA
- Kuendesha magari ya Abiria na Malori.
- Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri na usafi wakati wote na kufanya Uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
- Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari.
- Kutunza na kuandika daftari la Safari “Log – book” kwa Safari zote.
SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi daraja la II.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya serikali yaani TGS B1 yaani Tsh. 450,000/= kwa mwezi.
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 1
KAZI ZA KUFANYA
- Kuwa Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
- Kuwa Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu mbalimbali za Serikali.
- Kuandaa Taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
- Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika Kijiji.
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
- Kuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji.
SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali yaani TGS B1 yaani Tsh. 450,000/= kwa mwezi.
Kuona Nafasi zaidi za Kazi Mbeya Distric May 2023 Donwload PDF Bonyeza Hapa
NAFASI za Kazi Mbeya Distric May 2023, Nafasi za kazi wiki hii,NAFASI ZA KAZI Mbeya Distric,Mbeya Distric jobs,Nafasi za kazi 2023, Nafasi za Kazi Wilaya ya Mbeya May 2023,Nafasi za Kazi Mbeya Distric Leo May 2023.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Mbeya Distric jobs, Nafasi za kazi 2023, NAFASI ZA KAZI Mbeya Distric, Nafasi za Kazi Mbeya Distric Leo May 2023., NAFASI za Kazi Mbeya Distric May 2023, nafasi za kazi wiki hii, Nafasi za Kazi Wilaya ya Mbeya May 2023