LIVE AL AHLY VS WYDAD AC Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 3:00 Usiku. 

NAFASI zaidi ya 1000 za Kazi Jeshi la Magereza Tanzania May 2023

Filed in Ajira, Michezo by on 10/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

NAFASI zaidi ya 1000 za Kazi Jeshi la Magereza Tanzania May 2023

NAFASI zaidi ya 1000 za Kazi Jeshi la Magereza Tanzania May 2023,Job Vacancies at Jeshi la Magereza Tanzania 2023,Mshahara wa jeshi la magereza,Nafasi za kazi Magereza 2023 PDF,Nafasi za kazi Magereza 2023,Kazi za JESHI LA MAGEREZA,Anuani ya jeshi la magereza,Anuani za magereza tanzania,Call For Work at Magereza 2023,Nafasi za kujiunga na jeshi la magereza 2023 Tanzania,Nafasi Mpya za Kazi Jeshi La Magereza | Tanzania Jobs 2023,https://magereza.go.tz, Nafasi Mpya za Kazi Jeshi La Magereza | Tanzania Jobs 2023,New Jobs Jeshi la Magereza Tanzania 2023.

NAFASI zaidi ya 1000 za Kazi Jeshi la Magereza Tanzania May 2023

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye ujuzi wa fani mbalimbali kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe ni raia wa Tanzania.
  • Awe na Kitambulisho cha Uraia au namba ya Utaifa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
  • Awe amehitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), waliopo makambini au waliohitimu mafunzo tajwa na kurejea uraiani.
  • Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini.
  • Awe na umri kati ya miaka 18-33.
  • Awe na cheti cha Kuzaliwa.
  • Awe na urefu usiopungua futi 5’4 kwa wanawake na futi 5’7 kwa wanaume.
  • Awe na siha na afya njema ya mwili na akili iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
  • Asiwe ameoa/kuolewa.
  • Asiwe na alama au michoro (tatoo) yoyote katika mwili wake.
  • Awe na nidhamu na tabia njema na awe hajawahi kupatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Magereza na kufanya kazi mahali popote nchini Tanzania.
  • Awe tayari kujigharamia yeye binafsi katika hatua zote za awali za usaili wa ajira hii hadi kuripoti mafunzoni.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Mwombaji anatakiwa kuandika barua yake ya maombi kwa mkono wake (handwriting) na namba yake ya simu ya mkononi anayoweza kupatikana muda wowote.

Pamoja na barua ya maombi anapaswa kuambatisha nyaraka zifuatazo:-

  • Barua ya utambulisho toka Mtendaji wa Kata au Serikali ya Mitaa/Kijiji anakoishi Mwombaji
  • Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya Utaifa (NIDA).
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa (birth certificate);
  • Nakala ya cheti cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au cheti cha Jeshi la Kujenga Uchumi ((JKU) au barua za utambulisho kutoka Mkuu wa Kikosi kwa wale waliopo makambini.
  • Fomu yenye taarifa za upimaji wa afya ya Mwombaji wa kazi
  • Nakala za vyeti vya elimu ya Sekondari (leaving & academic).
  • Awe na nakala za vyeti vya fani/ujuzi mbalimbali uliotangazwa
    (academic certificates and transcripts).
  • Awe na picha nne (4) za ‘passport size’.
  • Barua zote za maombi zitumwe kwa njia ya posta kwa anwani ifuatayo:-

Kamishna Jenerali wa Magereza,
Makao Makuu ya Magereza,
Barabara ya Arusha,
Eneo la Msalato,
S.L.P 1176,
DODOMA.

NB: Hakuna barua itakayopokelewa kwa njia ya mkono au barua pepe (E-mail).

Waombaji wote ambao walishafukuzwa katika kozi za Kijeshi za mafunzo ya awali ya Magereza hawaruhusiwi kuomba tena.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Mei, 2023.

NAFASI zaidi ya 1000 za Kazi Jeshi la Magereza Tanzania May 2023 Donwload PDF

WATAALAM WENYE FANI ZINAZOHITAJIKA MAGEREZA

  • Shahada ya Saikolojia (Bachelor Degree of Counselling, Social Work, Psychosocial).
  • Shahada ya Afya (Doctor of Medicine).
  • Shahada ya Famasia (Bachelor Degree in Pharmacy).
  • Shahada ya Mifugo (Bachelor of Science in Animal Science.
  • Shahada ya kilimo na Umwagiliaji (Bachelor of Science in Irrigation and Water Resources Engineering).
  • Shahada ya Kilimo (Bachelor of Science in Agronomy/Agriculture
    General/Horticulture).
    Shahada ya Misitu (Bachelor Degree in Forest);
  • Stashahada ya Ufugaji Samaki (Diploma in Aquaculture).
  • Stashahada katika Ufundi wa Vifaa vya Hospitali (Diploma in
    Electronics and Biomedical Engineering).
  • Stashahada ya Maabara za Hospitali (Diploma in Medical
    Laboratory Sciences).
  • Stashahada katika Radiografia ya Utambuzi (Diploma in Diagnostic Radiography).
  • Stashahada ya Afya ya Kinywa (Diploma in Clinical Dentistry).
  • Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine).
  • Stashahada ya Katibu Muhtasi na Kompyuta (Diploma in Personal Secretary and Computer).
  • Stashahada ya Sayansi ya Uchunguzi wa Kimtandao (Diploma in Forensic Sciences).
  • Astashahada ya Ufundi Vifaa vya Aluminium (Level II).
  • Astashahada ya Ufundi Ujenzi (Certificate of Tiling Level II).
  • Astashahada ya Mafundi wa Samani (Certificate of Cabinet Making Level II).
  • Astashahada ya Ufundi wa Uchomeleaji (Certificate of Welding & Fabrication Level II).
  • Astashahada ya Ufundi Bomba (Certificate of Plumbing and Pipe Fitting Level II).
  • Astashahada ya Kupiga Buruji na Brassband.
  • Astashahada ya Ufundi Rangi za Nyumba (Certificate of Painting and Decoration Level II).
  • Astashahada ya Ufundi wa Umeme (Certificate of Domestic
    Electrical Installation Level II).
  • Astashahada ya Ufundi Selemala (Certificate of Carpentry and Joinery Level II).
  • Astashahada ya Teknolojia ya Nishati ya ‘Solar’ (Certificate of Solar Technology and Solar Energy Appliances Level II).
  • Astashahada ya Ushonaji (Certificate of Tailoring, Designing and
    Suit Making Level II).
  • Astashahada ya Kudarizi (Certificate of Embroidery Level II).
  • Astashahada ya Mapambo (Certificate of Decoration Level II);
  • Astashahada ya Ufundi wa Viyoyozi na Mafriji (Certificate of Refrigeration and Air Condition Level II).

Imetolewa na:-
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Makao Makuu ya Magereza,
Barabara ya Arusha,
Eneo la Msalato,
S.L.P 1176,
DODOMA.

Job Vacancies at Jeshi la Magereza Tanzania 2023,Mshahara wa jeshi la magereza,Nafasi za kazi Magereza 2023 PDF,Nafasi za kazi Magereza 2023,Kazi za JESHI LA MAGEREZA,Anuani ya jeshi la magereza,Anuani za magereza tanzania,Call For Work at Magereza 2023,Nafasi za kujiunga na jeshi la magereza 2023 Tanzania,Nafasi Mpya za Kazi Jeshi La Magereza | Tanzania Jobs 2023,https://magereza.go.tz, Nafasi Mpya za Kazi Jeshi La Magereza | Tanzania Jobs 2023,New Jobs Jeshi la Magereza Tanzania 2023.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *