Nijuze Habari

NBC Mdhamini mpya Ligi Kuu Tanzania Bara

Filed in Michezo by on 07/10/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF, na Benki ya NBC zimeingia makubaliano ya Mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara na msimu huu benki hiyo itatoa kitita cha Bilioni 2.5 kabla ya makato ya VAT.

Akizungumza jana Octoba 6, baada ya kuingia makubaliano hayo ,Rais wa TFF,  Wallece Karia amesema wameingia makubaliano na NBC baada ya mchakato wa muda mrefu ambao ulikuwa na lengo la kuwekeza vizuri katika mchezo wa mpira wa miguu, Karia amesema kuanzia sasa Ligi Kuu inatambulika NBC Tanzania Premier League.

Amesema wamepata udhamini kutokana na Shirikisho  kuaminiwa na taasisi mbalimbali kutokana na kuwa na Utawala bora pamoja na uadilifu katika rasilimali fedha na kuzipeleka katika maeneo yaliyoekezwa kwa maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu.

Ameongeza kuwa pesa hizo zinapelekwa katika Bodi ya Ligi, ambao ndio waendeshaji wa Ligi na kubwa zaidi wamedhamiria kuhakikisha pesa hiyo itatumiwa na vilabu katika kukidhi masuala ya usafiri ambao umekuwa changamoto kwa baadhi ya vilabu.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema wao kama wadau wa michezo wamevutiwa na maendeleo ya Ligi Kuu ambayo imekuwa na ushawishi na kufanya vizuri katika viwango vya ubora barani Afrika.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.