Nijuze Habari App

NBC yatambulisha Kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Filed in Michezo, New by on 08/06/2023 0 Comments
Share This
 

SHINDA 50,000 BURE KILA SIKU BONYEZA HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

NBC yatambulisha Kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Wakati Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2022/2023 ikifikia tamati Ijumaa hii ya Juni 9, 2023, Mdhamini Mkuu wa Ligi hiyo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi Kombe jipya la Ligi Kuu lililoboreshwa.

Kombe hilo limezinduliwa Jumatano ya Juni 7, 2023 Jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa Habari na litakabidhiwa kwa Bingwa mtetezi ambaye ni Young Africans ya Jijini Dar es Salaam ambao wamekwisha tangazwa Washindi.

NBC yatambulisha Kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

NBC yatambulisha Kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Wakati Yanga ikikabidhiwa Kombe hilo, tayari timu mbili za Polisi Tanzania na Ruvu Shooting tayari zimeshuka daraja, huku nafasi ya pili inashikwa na Simba SC ya Jijini Dar es salaam pia.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Benki hiyo, Godwin Semunyu amesema kuwa NBC ikiwa kama Mdhamini Mkuu wa Ligi imeboresha Kombe kutokana na maoni ya wadau mbalimbali wa Soka.

Amesema kuwa NBC ikiwa Mdhamini Mkuu wa Ligi ya Tanzania Bara, inajivunia Mafanikio Makubwa ya Ligi yetu.

“Kwa sasa Ligi yetu ni ya tano kwa Ubora Afrika na hii ni hatua kubwa na nzuri kwa soka letu. Leo tumezindua Kombe lililoboreshwa ikiwa pia ni sehemu ya kuongeza thamani kwa Ligi yetu,” alisema Semunyu.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Semunyu ameongeza kuwa ikiwa ni sehemu ya Maboresho ya Ligi, Benki ya NBC inatoa Bima kwa Wachezaji wote wa Ligi Kuu pamoja na Familia zao pamoja na mikopo ya Mabasi kwa timu zinazoshiriki Ligi.

“Ili kuongeza hamasa kwa wachezaji na makocha, tunatoa tuzo mbalimbali kwa makundi haya kila mwezi,” amesema

“Benki ya NBC itaendelea kutoa mchango wake katika kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini kwa kuwa inatambua umuhimu na mchango wa michezo kwa maendeleo,” alisema Semunyu

Naye Mkurugenzi wa Fedha wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayela amesema kuwa Udhamini wa NBC umekuwa wenye tija kubwa kwa Ligi na NBC ni mdau mkubwa katika maendeleo ya Soka hapa nchini.

“Leo Tanzania tunajivunia Ligi yetu kuwa moja katika Ligi Bora Barani Afrika tukishikilia nafasi ya tano. Tunaishukuru sana Benki ya NBC kwa Udhamini wake ambao umesaidia kufika hapa tulipo huku tukisonga mbele kwa kujiamini,” alisema Mwayela.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *