Nijuze Habari App

PICHAZ: Yanga yakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa NBC 2022/2023

Filed in Michezo, New by on 09/06/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

PICHAZ: Yanga yakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa NBC 2022/2023

PICHAZ: Yanga yakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa NBC 2022/2023

PICHAZ: Yanga yakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa NBC 2022/2023

MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2022/2023 Young Africans wamekabidhiwa Kombe lao leo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele dakika ya 33 na Yanick Bangala Litombo dakika za ngongeza baada ya zile 90 kuisha.

Klabu hiyo imekamilisha msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC kwa pointi 78, pointi tano zaidi ya Simba SC waliomaliza nafasi ya Pili, huku Azam FC ikimaliza nafasi ya tatu kwa pointi 59, pointi nne zaidi ya Singida Big Stars waliomaliza nafasi ya nne na Namungo FC iliyomaliza na pointi 40 inakamilisha timu tano Bora Msimu huu wa 2022/2023.

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele aliyemaliza na mabao ya 17, sawa na Saido Ntibanzokiza w Simba wote wanakuwa Wafungaji Bora wa Msimu huu wa 2022/2023.

Matokeo ya mechi zingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo Ijumaa tarehe 09 June 2023 za kufunga msimu wa 2022/23, Simba imeichapa Coastal Union mabao 3-1, mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Saido Ntibanzokiza mawili, dakika ya 12 na 73 na John Bocco dakika ya 55, wakati la Coastal Union limefungwa na Mbaraka Hamza kwa penati dakika ya 6.

Nayo Azam FC imeibuka na Ushindi mnono wa mabao 8-0 dhidi ya Polisi Tanzania, mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na Prince Dube manne na mengine Kipre Junior, Iddi Nado mawili na Yahya Zayd.

Mechi nyingine, KMC imeichapa Mbeya City bao 1-0, mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mtibwa Sugar wao wamepata Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Ihefu nao wameshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.

Namungo ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars.

Nayo Dodoma Jiji imepata Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Katika hatua nyingine, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania zimeshuka Daraja moja kwa moja wakati Mbeya City na KMC zitacheza mechi mbili nyumbani na ugenini kuwania kubaki Ligi Kuu msimu ujao wa 2023/2024.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Mshindi wa jumla mechi hizo mbili kati ya Mbeya City na KMC itabaki Ligi Kuu na itakayofungwa itakwenda kucheza na Mashujaa FC ya Kigoma kuwania kubaki Ligi Kuu.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *