Nijuze Habari

PITSO Mosemano afunguka mengi kwenye Mkutano na waandishi wa habari

Filed in Michezo by on 05/08/2022 0 Comments

PITSO Mosemano afunguka mengi kwenye Mkutano ba waandishi wa habariPitso Mosemano, Mkufunzi wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly, yuko Tanzania kwa mwaliko maalum kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi

Nijuze Habari Application

PITSO Mosemano afunguka mengi kwenye Mkutano na waandishi wa habari

PITSO Mosemano afunguka mengi kwenye Mkutano ba waandishi wa habariPitso Mosemano, Mkufunzi wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly, yuko Tanzania kwa mwaliko maalum kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi

Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari, Mosimane amesema kuwa amefurahiq kuja Tanzania kujifunza mambo mengine nje ya soka.

Mosimane amesema kama mwafrika, anaunga mkono jambo jema linalofanywa na waafrika wenzake.

Aidha Mosimane amesema alivutiwa zaidi ya ‘Parade’ iliyofanywa na Yanga baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu

“Nilishangazwa na wingi wa mashabiki waliojitokeza kusherehekea Ubingwa, ni tukio ambalo linaonyesha ni kwa kiasi gani Waafrika nasi tunaweza kufurahia matukio yetu”

“Yanga sio timu kubwa tu Tanzania, bali Afrika sote tunaifahamu. Najua mnaingia kwenye michuano ya CAF, najua mtafanya vizuri, kocha unapaswa kushinda mechi zote za nyumbani na kupata droo mbili ugenini inatosha. Nimekuwa katika mashindano hayo kwa miaka 12, nadhani inawezekana”

“Kwa sasa niko mapumziko, niliamua kusitisha mkataba wangu na Al Ahly, nilikuwa na mkataba wa miaka miwili lakini kwa sasa nahitaji kupumzika”

“Haikuwa rahisi mimi kuondoka Al Ahly lakini ilikuwa ni lazima niondoke nipate mapumziko, nimefanya kazi hii kwa miaka 21 pasipo mapumziko,” alisema Mosimane.

Pichani ni Pitso Mosimane akitoa mafunzo ya soka kwa vijana wadogo leo asubuhi Viwanja vya Gymkhana kuelekea Siku ya Mwananchi kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.Pitso Mosimane Yanga SC

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.