RAIS Dkt.Samia afanya Uhamisho na Uteuzi Wakuu wa Mikoa na Wilaya

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


RAIS Dkt.Samia afanya Uhamisho na Uteuzi Wakuu wa Mikoa na Wilaya

RAIS Dkt.Samia afanya Uhamisho na Uteuzi Wakuu wa Mikoa na Wilaya
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya Mabadiliko madogo ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa, uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 23, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Mhe. Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mtanda anachukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Pia, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Mhe. Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anachukua nafasi ya Mhe. Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.
Aidha, Mhe. Charles Makongoro Nyerere amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Mhe. Nyerere ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mhe. Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Manyara.
Wakati huo huo,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo. Anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huu unaanza mara moja.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uapisho wa Mkuu wa Mkoa mpya utafanyika tarehe 24 Mei, 2023 saa 10:00 jioni, Ikulu Chamwino.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ADA za LIPA kwa Airtel Mitandao Yote
- TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024
- YANGA yashika Nafasi ya 9 Simba ya 10 Afrika 2022/2023
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- Ada zaAirtel Money 2022/2023 | Makato mapya ya Airtel Money
- ADA Mpya za Tigo Pesa (Tigo Pesa Tariffs 2022/2023)
- Ada/Makato ya HaloPesa Tanzania, Halopesa Tariffs 2023
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: RAIS Dkt.Samia afanya Uhamisho na Uteuzi Wakuu wa Mikoa na Wilaya