Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

Filed in Habari by on 27/04/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 376 huku sita kati yao wakiachiwa huru na wengine watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa msamaha huo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao uliwezesha kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (jana) Aprili 26, 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni.

“Wafungwa 376 watanufaika na msamaha huu ambapo sita wataachiwa huru leo (jana) Aprili 26, 2023 na 370 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

“Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani,”amefafanua Mheshimiwa Waziri Mhandisi Masauni.

Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

Amefafanua kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa msamaha huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Waziri Mhandisi Masauni amefafanua kuwa,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa msamaha huo kwa wafungwa kwa masharti kadhaa.

Mosi, wafungwa wenye sifa stahiki wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya Kifungu cha 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58.

“Wafungwa hao sharti wawe wamehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka mitatu ambao wametumikia robo ya adhabu zao gerezani na wawe wameingia gerezani kabla ya Februari 26, 2023 isipokuwa wafunguwa walioorodheshwa katika sharti la 2 (i-x).

Rais Dkt.Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376 April 2023

“Wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na watoto wadogo wanaonyonya na wasionyonya,”amefafanua Mheshimiwa Waziri Mhandisi Masauni.

Pili, msamaha huo hauwahusishi wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na wenye makosa ya kujaribu kuua, kujaribu kujiua au kuua watoto wachanga (attempt to murder, attempt suicide or infanticide).

Wafungwa wengine ambao hawanufaiki na msamaha huo ni wale ambao wanatumikia vifungo vya nje chini ya Sheria ya Bodi za Paroli Sura ya 400 (R.E 2002), Sheria ya Huduma kwa Jamii Sura ya 291 (R.E 2002) na Kanuni za Kifungo cha Nje (The Prisons (Extra Mural Penal Employment Regulations, 1968).

Aidha, wengine ni wafungwa aliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa mashauri au kesi za uhujumu uchumi na wale wanaotumikia vifungo kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka, utakatishaji wa fedha, rushwa, usafirishaji na kujihusisha kwa namna yoyote ile na dawa za kulevya.

Pia, wengine ni wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kujamiiana, utekaji au wizi wa watoto, kupoka, kuwapa mimba wanafunzi au makosa yoyote yale yanayohusiana na ukatili dhidi ya watoto na kujihusisha kwa namna yoyote ile na biashara haramu ya binadamu.

Aidha, wengine ambao hawanufaiki na msamaha wa Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa Mheshimiwa Waziri Mhandisi Masauni, ni wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo kwa makosa ya kukutwa na viungo vya binadamu, unyang’anyi, unyang’anyi wa kutumia nguvu, unyang’anyi wa kutumia silaha, kumiliki silaha, risasi, milipuko au kujaribu kutenda makosa hayo.

Amesema, pia wafungwa ambao hawanufaiki na msamaha ni wale ambao wanatumikia vifungo kwa makosa ya wizi au ubadhirifu wa fedha au mali za Serikali.

Katika hatua nyingine, wengine ambao hawanufaiki ni wale ambao wanatumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali au kusaidia kutendeka kwa makosa hayo.

“Wengine ni wafungwa warudiaji na wale waliowahi kupata msamaha wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo wafungwa wa madeni (civil prisoners),”amefafanua Mheshimiwa Waziri Mhandisi Masauni kupitia taarifa hiyo.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *